Wagombea
wa nafasi ya Rais wa ZIFASO Juma Shirazi Hassan a Makamu wake Zuwena
Jaku Hassan (wa katikati) wakiongozwa kuingia katika kampasi ya Chuo cha
Uongozi wa Fedha Zanzibar kiliopo Chwaka Mkoa Kusini Unguja tayari kwa
ajili ya kupiga kura.
Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi ya wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar
Sabrina Yussuf Shaaban akielezea juu ya utaratibu mzima wa kupiga kura
ili kupata viongozi wapya wa ZIFASO .
Mlezi
wa wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar Maalim Wazir Hamad
akitoa nasaha zake kwa wapiga kura ambao ni wanafunzi wote wa chuo
hicho.
Mgeni
rasmi katika uchaguzi huo ambae ni Afisa kutoka Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (ZEC) Mohd Ali Abdalla akiwanasihi wasimamizi na wapiga kura
kuendesha uchaguzi katika misingi ya haki.
Mgombea
pekee wa nafasi ya Rais wa ZIFASO Juma Shirazi Hassan akipiga kura
yake katika uchaguzi huo uliofanyika chuoni Chwaka Mkoa Kusini Unguja.
0 maoni:
Chapisha Maoni