Jumanne, 26 Aprili 2016

JESHI LA POLISI MKOA WA KILIMANJARO LANASA BHANGI MISOKOTO 4500,BASTOLA PAMOJA NA ZANA NYINGINE


Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,kamishna msaidizi ,Wilbroad Mutafungwa akionesha misokoto ya Bhangi iliyokamatwa baada ya wahusika kufanikiwa kuwakimbia askari Polisi.
Kamnad wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,kamishna msaidizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa akionesha misokoto 4500 pamoja na kilogramu 10 za bhangi ambayo haijasokotwa iliyokamatwa wilaya ya Siha baada ya wahusika kuitelekeza.
Sehemu ya Bhangi iliyokamatwa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Wilbroad Mutafungwa akionesha vifaa mbalimbali yakiwemo mapanga na mashoka yaliyokuwa yakitumika katika utekaji wa magari wilayani Mwanga.
Baadhi ya vitu mbalimbali walivyokamtwa navyo watuhumiwa wa ujambazi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Wilbroad Mutafungwa akionesha bastola ambayo inadaiwa kutumika katika kufanyia uharifu.
Kamanda wa Polisi akiwaonesha watuhumiwa wa usafirishaji wa Mirungi namna ambavyo wamebuni mbinu mpya ya kusafirisha dawa hizo za kulevya.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa za kamanda Mutafungwa.
Baadhi ya askari Polisi pia walikuwepo kuimarisha usalama katika chumba cha mikutano katika ofisi ya kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro.
 
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

0 maoni:

Chapisha Maoni