Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
……………………………………………..
WANANCHI
wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar, wametakiwa kujenga tabia ya kufanya
usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kuepuka maradhi ya kipindupindu
yanayoathiri maeneo mbali mbali nchini.
Wito
huo umetolewa kwa nyakati tofauti na Mbunge wa jimbo la Kikwajuni,
Muandisi Hamad Yussuf Masauni alipokuwa akifanya usafi wa mazingira
katika maeneo mbali mbali ya jimbo hilo Mjini hapa.
Alisema
maeneo mengi ya jimbo hilo hasa katika Majumba ya Maendeleo ya
Michenzani ni machafu sana hali inayoweza kusababisha maradhi ya
miripuko yakiwemo kipindupindu na kichocho.
Masauni
ambaye pia ni Naibu Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, alieleza kuwa
wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi
wa mazingira na kupelekea uharibifu wa miundombinu ya kusafirisha maji
taka ikiwemo mitaro kuziba.
“
Nachukua fursa hii kuwakumbusha wananchi wa kikwajuni kuwa suala la
usafi wa mazingira halina itikadi za kisiasa ni lazima wananchi sote
tuungane bila ya kujali tofauti za kisiasa.
Pia
nakuombeni wananchi hasa mnaoishi katika majumba ya michenzani
mbadilike kwa kujali mazingira yenu kwani mjue kuwa endapo eneo hili
litapata maradhi ya mripuko kuna hatari ya wananchi wengi kupoteza
maisha kwa maradhi ambayo tuna uwezo wa kuyazuia.”, alisema Masauni huku
akisisitiza umuhimu wa kufanya usafi wa mara kwa mara katika maeneo
hayo.
Alisema
viongozi wa jimbo hilo kwa sasa wanapanga kuanzisha kikundi maalum cha
vijana wa kufanya usafi katika maeneo ya jimbo hilo, ambapo kila
kaya(nyumba) watakuwa wanachangia kiasi cha shilingi 200 kila siku ili
fedha hizo ziweze kuwasaidia watu wanaofanya usafi huo.
“Aibu
kubwa kuona ndani ya jimbo la kikwajuni panaanza kupatikana wagonjwa wa
maradhi ya kipindupindu kwani ni jimbo lenye sifa ya usafi na ukaribmu
toka enzi na enzi tena lipo mjini, lazima tushirikiane kufanya usafi
katika maeneo yetu.” Alisema Masauni.
Aidha
aliishauri Manispaa ya Zanzibar kuanza mara moja utafti wa kubaini
mifumo ya maji machafu na masafi inayoingiliana katika maeneo hayo ili
kuifanyia matengenezo kwa haraka kabla hapajatokea maafa ya maradhi ya
miripuko na kusababisha athari kwa wananchi wa maeneo hayo.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salum Ali(Jazeera)
aliwapongeza wananchi wa jimbo hilo waliojitokeza kufanya usafi wa
mazingira kwa lengo la kuweka maeneo yako katika hali ya usafi.
Jazeera
alisema kwamba kinga ya maradhi ya mripuko hasa kipindupindu ni usafi
wa mazingira hivyo kila mwananchi anatakiwa kutekeleza wajibu wake bila
ya kulazishwa na mtu.
Naye
Mkurugenzi wa Manispaa ya Zanzibar, Aboud Hassan Serenge alisema kila
mwananchi ana jukumu la kufanya usafi wa mazingira katika maeneo
anayoishi kwa lengo la kuweka mji wa Zanzibar katika hali ya usafi.
Serenge
alifafanua kwamba kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakichafua mazingira
ya mji kwa makusudi huku wakidai kuwa Manispaa ipo na ndiyo yenye
dhamana ya kufanya usafi jambo ambalo sio sahihi kwani kila mtu suala la
usafi linamuhusu.
Mkurugenzi
huyo alieleza kuwa endapo wananchi wa manispaa ya Zanzibar wataendelea
kushirikiana vizuri na mamlaka hayo katika kuweka mjini wa Zanzibar
katika hali ya usafi, basin chi itarudi katika historia ya haiba na
usafi uliotukuka kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Alisema
Manispaa ina mpago wa kufanya marekebisho katika maeneo mbali mbali ya
mji wa Zanzibar yanayoonekana kuwa na tatizo la kuziba kwa mitaro na
mifereji ya maji machafu inayopita chini kwa chini ili kuzuia uchafu
unaosambaa katika maeneo mbali mvali ya mji huo.
0 maoni:
Chapisha Maoni