Na Mwandishi Wetu
BONDIA Lulu Kayage yupo katika
mazoezi mazito na makali kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake wa
kimataifa na Chiedza Homakoma ‘Nikita’ Malawi mpambano utakaofanyika mei
14 katika uwanja wa ndani wa Taifa
Akizungumza wakati wa mazoezi
yake anayofanya Kinondoni Msisiri amesema anajiandaa vizuri tu kwa ajili
ya kumkabili mmalawi huyo atakaepigana nae aliongeza kwa kusema unajua rekodi yangu imeharibika kidogo kwa kuwa nilipigwa kwa pointi katika pambano langu la mwisho
Hivyo nimejipanga vizuri
kuhakikisha nafanya vema katika mpambano huo wa kimataifa na ninawahidi
mashabiki wagu kuwa siku hiyo nitakuwa radhi kufia ulingoni ili ushindi
ubaki Tanzania na siwezi kupigwa hapa nchini nitatia aibu Taifa langu.
Siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mbalimbali ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi nchini
ambapo bondia Thomas Mashali atakumbana na Sajjad Mehrab kutoka ‘Irani’ ubingwa wa Dunia mkanda wa U.B.O
Mapambano mengine ya kimataifa
yatawakutanisha bondia Ramadhan Shauri atakayepambana na Osgood Kayuni
wa Malawi wakati Twaha Kassim atapambana na Fred Nyakese kutoka Kenya
na Saleh Mkalekwa atakumbana na Jems Onyango wa Kenya huku Francis
Miyeyusho akivaana na Frank Kiwalabye wa Uganda naye Nassibu Ramadhani
atacheza na Edward Kakembo wa Uganda
Mapambano mengine ni kati ya Shaban Kaoneka atakayecheza na Hassan Mwakinyo na Issa Nampepeche atakumbana na Baina Mazola
Mapambano hayo ya kimataifa yameandaliwa na promota mkongwe Ally Mwazowa kutoka mkoa wa Tanga
siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazo sindikiza mapambano hayo ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi
0 maoni:
Chapisha Maoni