Mkuu wa wilaya Iringa
Richard Ksesela ashiriki kufunga mfunzo
ya PUBLIC PRIVATE DIALOGUE (PPD) pamoja na kugawa vyeti kwa washiriki.
Mafunzo hayo yanaendeshwa
na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam- Shule
ya Boiashara (UDBS) na kudhaminiwa na mradi wa BEST-PPD.
Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo yaliyofanyika
mkoani Iringa na kufungwa leo hii[jana]yaliyohudhuliwa
na wilaya za Njombe,Iringa,Kilolo na Mufindi alisisitiza kudumisha
nidhamu katika kazi ili kuleta ufanisi
mahali pa kazi,hasa katika sekta binafsi.
Katika hotuba
yake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard kasesela aliyoitoa wakati akifunga, aliwataka
washiriki kuyafanyia kazi yale waliyoyapata ili kuleta chachu ya maendeleo katika
wilaya wanazotoka, jamii,na Taifa kwa ujumla.
Kasesela alisema mafunzo
yaliyotolewa ni muhimu sana kwa Taifa letu na yana lengo la kuhimiza mijadala
na mazungumzo kati ya sekta binafsi na serikali kwa ujumla.
Katika hotuba yake alisisitiza
sana suala la nidhamu, na kusema kuwa nidhamu ndiyo msingi wa kujenga sekta
binafsi iliyo imara. Pia aliwaasa kupunguza utitili wa jumuiya za sekta
bianfsini muhimu zikaungana na kujenga moja yenye nguvu kwa maendeleo ya Taifa.
Aidha alitoa ushauri
kwa halmashauri zote nchini kufungua
dawati kwa ajili ya mijadala na sekta binafsi ili ziweze kutekeleza majukumu
mengine kwa niaba ya serikali.
‘’’’’’’’’’’’’’’’’Bila
sekta binafsi imara uchumi wa nchi hauwezi kukua, ni muhimu sekta binafsi
ikaanza kuchukua nafasi stahiki ikiwemo kutekeleza majukumu mengine kwa niaba
ya serikali mfano ukuaji wa michezo mabayo inahitaji uwekezaji ili serikali
iondokane na kuwekeza, nchi kama Marekani hazina wizara ya michezo"
alisema.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni