Mkuu wa mkoa Iringa Amina Masenza akizungumza wandishi wa habari hawapo pichani kufuatia mgomo wa wananchi wanatakiwa kupisha makazi yao kwa ajili ya ujenzi wa barabara
Wananchi wanaoishi eneo la Kihesa
ndani ya Manispaa ya Iringa wamelalamikia kitendo cha serikali
kuchelewa kuwalipa fidia baada ya eneo lao kuingizwa kwenye mradi wa
ujenzi wa barabara ya mchepuko inayounganisha barabara kuu ya Dodoma Iringa
na ile ya Dar es Salaam Mbeya kupitia Iringa.
Barabara hiyo ya mchepuko
imebuniw ana serikali lengolikiwa kuondoa msongamano wa magari katika kati
yamji wa Iringa na pia kuwezesha magari yote ya abria kuifikia Stand Kuu ya mabasi
inayotarajia kujengwa eneo la Igumbilo nje kidogo ya Mji wa Iringa.
Wananchi hao jana waliandaamana
kimya kimya hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo walitaka kupewa ufafanuzi
kutoka serikalini juu ya hatima ya nyumba na mali zao baada ya nyumba
hizo kuanza kuharibika kutokana na kutofanyiwa ukarabati kwa muda mrefu.
Mwenyekiti wa umoja wa waathirika
hao Stanford Mwakasala alisema wao wameathirika kutokana na kuchelewa kulipwa
fidia hiyo baada ya ardhi yan Nyumba walizokuwa wakimiliki kufanyiwa uthamani
tangu mwaka 2012 na waokuziwa kuziendeleza hadi sasa.
“Tangu ufanyike uthamini hadi leo
hatujui hatima yetu,tumeandika barua kwa waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa lakini hatujapata ushirikiano na
tumefika hapa kutaka kupata ufafanuzi wa kilio chetu”alisema Mwakasala.
Naye Herieth Magambo alisema
kitendio cha kuchelwa kup;ipwa fidia kimewarudisha nyuma kimaendeleo kutokana
na nyumba zao kutowaingizia kipato kwa kipindi cha miaka minne.
“Nyumba zile zimekosa wapangaji kwani
wanaogopa kuingia na kuishi humo kutokana na kupigwa alama za X lakini kwa
wale wanaoendelea kuishi kwenye nyumba hizo wanatulazimisha kufanya ukarabati
ambao ni hasara kwetu kwani tayari zilishafanyiwa uthamini”alisema Magambo.
Akizungumza na wananchi hao Mkuu
wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema “Nimesikia kilio chenu na hata mimi
nilikuwa nalia pamoja nanyi,ninawahakikishia kuwa serikali itawalipa
fidia zenu pamoja na gharama za usumbufu”alisema.
Masenza alifafanua kuwa wananchi
hao wamechelewa kulipwa kutokana na kukosekana kwa fedha serikalini huku
serikali ya awamu ya Tano Dk John Magufuli ikianza kazi wka kugeukia sekta ya
elimu ambayo nayo inakabiliwa na changamoto.
Alisema wananchi hao watalipwa
fedha zao katika bajeti ya mwaka huu ambayo tayari bunge limeanza kuijadili
bajeti hiyo mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa umoja wa wananchi
hao Frank Mwaisumbe alimshukuru Mkuu wa mkoa wa ahadi hiyo na kuongez akuwa
wao wanaimina naye kwa madai kuwa ndiye mwakilishi wa rais mkoani hapa.
mwisho
|
0 maoni:
Chapisha Maoni