Rais wa Shirikisho la
Soka Nchini (TFF) Jamal Malinzi akiongoza ujumbe wa maofisa wengine
wawili wa shirikisho hilo wamefanya ziara makao makuu ya ofisi za TBL
Group zilizopo Masaki jijini ambapo walikutana na mkurugenzi wake Mkuu
Roberto Jarrin na kufanya naye mazungumzo.
Ziara hiyo imeelezwa kuwa ina
lengo la kudumisha uhusiano miongoni mwa taasisi hizo mbili hususani
katika kuendeleza mchezo wa soka nchini.
Rais wa shirikisho la Mpira wa
Miguu Nchini (TFF) Jamal Malinzi (wa pili kulia ) Katibu Mkuu
shirikisho hilo, Mwesigwa Selestine (kushoto) na Mjumbe wa Kamati ya
TFF Richard Sinamtwa (katikati) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu
wa TBL Group Roberto Jarrin (Kulia ) wakati walipofanya ziara ya kikazi
ofisini kwake Masaki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL GROUP
Roberto Jarrin (wapili kushoto) Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu
Nchini (TFF) Jamal Malinzi (wa pili kutoka kulia) Katibu Mkuu
shirikisho hilo , Mwesigwa Selestine (kulia) na Mjumbe wa Kamati ya
TFF, Richard Sinamtwa (kushoto )wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati
walipotembelea katika ofisi za TBL Masaki jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa TBL GROUP
Roberto Jarrin (katikati akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya TFF,
Richard Sinamtwa , Kulia ni Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini
(TFF) Jamal Malinzi
0 maoni:
Chapisha Maoni