hewa,” alisema Hugh Richmond, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara, Clarke Energy. “Huu ukiwa kama mradi wa kwanza wa kampuni yetu nchini Tanzania, utasaidia kupunguza gharama ya kiwanda kujiendesha huku ukifua umeme wa kuaminika utakaotosheleza mahitaji,” alisema Richmond.
Ufungaji wa mtambo huu utaiwezesha Kampuni ya Bakhresa kutumia gesi hii mpya kupata nishati za umeme na joto kwa ufanisi na uhakika. Kampuni ya Clarke Energy huuza kwa niaba ya GE aina ya injini ya gesi Jenbacher J612 yenye uwezo wa kuzalisha megawati 1.82 (MW) za nishati ya umeme. Mtambo huu utazalisha pia nishati ya joto ambayo itaingizwa kwenye jiko la mvuke lenye uwezo wa kuzalisha kilowati 1,040. Clarke Energy itakua mvumbuzi kwa kuzalisha nishati ya umeme na joto ambapo hili litafanikiwa kwa kufunga mitambo ya umeme kwenye gridi ya taifa ili kuweza kubeba mzigo wa kilovolti 33”.
gepower
Injini ya gesi ya GE aina ya Jenbacher ambayo itauzwa kwa kampuni ya Said Salim Bhakhresa ili kupunguza gharama za uendeshaji.
“Injini za mtambo wa gesi aina ya Jenbacher J612 huzalisha hewa chafu kidogo, ila huzalisha umeme kwa ufanisi wa hali ya juu,” alisema Oluwatoyin Abegunde, Mkuu wa Biashara GE Distributed Power kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa nishati katika Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika. Alisema,” Kwa kuchanganya teknolojia yetu ya uhakika na utaalamu wa Kampuni ya Clarke Energy, kwa pamoja tutazalisha umeme wa uhakika pamoja na suluhisho la kupunguza gharama kwa Kampuni ya Bakhresa na hivyo kuwasaidia kuwa mbele ya viwanda vingine nchini Tanzania.”
Kampuni ya Bakhresa, ni moja ya viwanda vinayoongoza nchini Tanzania na Afrika Mashariki ambayo ilizinduliwa mwaka 1970. Leo hii familia ya viwanda vya Bahkresa imezidi kujizolea umaarufu kibiashara katika Ukanda wa Afrika Mashariki zikiwamo nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi. Pia nchi za Malawi, Msumbiji na Afrika Kusini. Tayari kuna makampuni kadhaa chini ya mwamvuli wake na imewekeza hasa kwenye sekta ya vinywaji, ufungaji vifaa, huduma za baharini, mafuta ya petroli na burudani.