Mwenyekiti
wa MISATAN, Simon Berege akizungumza na waandisshi wa habari kuhusu
SIku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari. Kushoto ni Afisa Mafunzo wa TMF,
Raziah Mawanga na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri na Makamu
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile.
Siku
za Uhuru wa Vyombo vya Habari ambayo hufanyika Mei 3 ya kila mwaka
inataraji kufanyika jijini Mwanza kwa mwaka huu ambapo mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman na
kuhudhuliwa na viongozi wengine nchini na wengine kutoka nje ya nchini
ambapo kwa mwaka huu kaulimbiu ni KUPATA TAARIFA NI HAKI YAKO YA MSINGI.
Akizungumzia
sherehe hizo katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa
MISATAN, Simon Berege amesema sherehe za mwaka huu zinataraji kuwa na
wageni zaidi ya 250 akiwepo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Mhe. Nape Nnauye, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,
Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues.
Aidha
Berege amesema kuwa siku ya uhuru wa vyombo vya habari kwa mwaka huu
itafanyika kwa siku mbili, Mei, 2 kutakuwa na kongamano ambalo
litatumika kujadili hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini na Mei, 3
ndiyo itakuwa siku husika ya maadhimisho.
“Kikawaida
huwa kuna mambo tunafanya katika siku hiyo, tutawakumbuka waandishi wa
habari waliopoteza maisha kazini, tutawakumbuka waandishi wa habari
maveterani na waandishi wa habari waliopatwa na matatizo wakiwa kazini
... kwa mwaka huu tutakuwa na mambo ya kipekee tofauti na miaka
iliyopita,” amesema Berege.
Pia
ameongeza kuwa watapitia sheria zinazohusu uhuru wa vyombo vya habari
kama Cyber Crime Act 2015 na Sheria ya Takwimu 2015 pia kuipitia
miswada ya huduma ya vyombo vya habari na uhuru wa kupata taarifa.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la
JAMHURI na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus
Balile akizungumzia hali ya uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata
taarifa ilivyo nchini. Kulia ni Afisa Mafunzo wa TMF, Raziah Mawanga,
Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege na Ofisa Miradi katika Kitengo cha
Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizelege.
Afisa Mafunzo wa TMF, Raziah
Mawanga akizungumza jinsi TMF inawasaidia waandishi wa habari ili waweze
kufanya kazi zao kwa weledi. Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la
Jamhuri na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus
Balile. Kulia ni Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege na Ofisa Miradi
katika Kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizelege.
Ofisa Miradi katika Kitengo cha
Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizelege akizungumzia ushiriki wa
UNESCO katika kuandaa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ambapo kwa
mwaka huu zinafanyika Mwanza. Kushoto ni Mwenyekiti wa MISATAN, Simon
Berege na Afisa Mafunzo wa TMF, Raziah Mawanga.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari
cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma-Ledama akieleza kazi za Umoja
wa Mataifa ili kuvisaidia vyombo vya habari kupata uhuru wa kufanya kazi
bila kuingiliwa.
Baadhi ya waandishi wa habari na watumishi waliohudhuria mkutano huo.
0 maoni:
Chapisha Maoni