Alhamisi, 28 Aprili 2016

WANANCHI KIHESA WALALAMIKA KUTOLIPWA FIDIA WAANDANAMA KWA RC

Wananchi wanaoishi eneo la Kihesa ndani ya Manispaa ya Iringa wamelalamikia kitendo cha serikali  kuchelewa kuwalipa fidia baada ya eneo lao kuingizwa kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya mchepuko inayounganisha barabara kuu ya Dodoma Iringa na ile ya Dar es Salaam Mbeya kupitia Iringa.


Barabara hiyo ya mchepuko imebuniw ana serikali lengolikiwa kuondoa msongamano wa magari katika kati yamji wa Iringa na pia kuwezesha magari yote ya abria kuifikia Stand Kuu ya mabasi inayotarajia kujengwa eneo la Igumbilo nje kidogo ya Mji wa Iringa.

Wananchi hao jana waliandaamana kimya kimya hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo walitaka kupewa ufafanuzi kutoka serikalini  juu ya hatima ya nyumba na mali zao baada ya nyumba hizo kuanza kuharibika kutokana na kutofanyiwa ukarabati kwa muda mrefu.

Mwenyekiti wa umoja wa waathirika hao Stanford Mwakasala alisema wao wameathirika kutokana na kuchelewa kulipwa fidia hiyo baada ya ardhi yan Nyumba walizokuwa wakimiliki kufanyiwa uthamani tangu mwaka 2012 na waokuziwa kuziendeleza hadi sasa.

“Tangu ufanyike uthamini hadi leo hatujui hatima yetu,tumeandika barua kwa waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa   lakini hatujapata ushirikiano na tumefika hapa kutaka kupata ufafanuzi wa kilio chetu”alisema Mwakasala.

Naye Herieth Magambo alisema kitendio cha kuchelwa kup;ipwa fidia kimewarudisha nyuma kimaendeleo kutokana na nyumba zao kutowaingizia kipato kwa kipindi cha miaka minne.
“Nyumba zile zimekosa wapangaji kwani wanaogopa kuingia na kuishi humo kutokana na kupigwa alama za X lakini kwa wale wanaoendelea kuishi kwenye nyumba hizo wanatulazimisha kufanya ukarabati ambao ni hasara kwetu kwani tayari zilishafanyiwa uthamini”alisema Magambo.

Akizungumza na wananchi hao Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema “Nimesikia kilio chenu na hata mimi nilikuwa  nalia pamoja nanyi,ninawahakikishia kuwa serikali itawalipa fidia zenu pamoja na gharama za usumbufu”alisema.

Masenza alifafanua kuwa wananchi hao wamechelewa kulipwa kutokana na kukosekana kwa fedha serikalini huku serikali ya awamu ya Tano Dk John Magufuli ikianza kazi wka kugeukia sekta ya elimu ambayo nayo inakabiliwa na changamoto.

Alisema wananchi hao watalipwa fedha zao katika bajeti ya mwaka huu ambayo tayari bunge limeanza kuijadili bajeti hiyo mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa umoja wa wananchi hao Frank Mwaisumbe alimshukuru Mkuu wa mkoa wa ahadi hiyo na kuongez akuwa wao wanaimina naye kwa madai kuwa ndiye mwakilishi wa rais mkoani hapa.

0 maoni:

Chapisha Maoni