…………………………………………………………………..
Bodi ya Utalii Tanzania imekutana
na wadau wa Utalii wa Tanzania kwa lengo la kujadili namna
watakavyoweza kushirikiana katika kutangaza utalii wa Tanzania. Mkutano
huo uliohudhuliwa na viongozi wa vyama mbalimbali vya utalii vya
Tanzania; Shirikisho la Utalii Tanzania (TCT),
Chama cha Wamiliki wa Hoteli Tanzania (HAT), Chama cha Waendesha
Safari za Anga Tanzania (TAOA) na Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (TASOTA)
Aidha, katika mkutano huo wadau
waliweza kutambulishwa tovuti maalumu (Tourism Destination Portal),
ulioandaliwa na TTB kwa ajili ya kuboresha utangazaji wa utalii kupitia
TEHAMA. Tovuti hiyo inapatikana kwenye http://www.tanzaniatourism.com/en.
Mkutano huo ulifanyika tarehe 20/04/2016 katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Utalii, Dar Es Salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni