Mwanamuziki kutoka Marekani maarufu kwa muziki wa chapa Funk, Prince ameaga dunia.
Mwanamuziki huyo raia wa Marekani alipatikana ameaga dunia katika makazi yake ya huko Minneapolis.
Image copyrightGettyImage captionPrince
Alikuwa na umri wa miaka 57.
Prince alitawala chati za muziki kote duniani katika miaka ya 70 na
themanini kwa vibao vyake maarufu kama vile 'I Wanna Be Your Lover' na
'Little Red Corvette'.
Anasifika kwa ubunifu wake wa kutajika na kwa midundo iliyowaongoa wapenzi wa muziki kote duniani .
Image copyrightGettyImage captionPrince
alibuni chapa yake binafsi ya muziki uliokuwa na sauti na ala za
mchanganyiko wa muziki wa Rock na , funk na psychedelia''.
Prince alibuni chapa yake binafsi ya muziki uliokuwa na sauti na ala za
mchanganyiko wa muziki wa Rock na , funk na psychedelia''.
Muziki wake ulikuwa maarufu kiasi ya kwanza aliwahi kuuza takriban albamu milioni 100.
Kipawa chake kilimwezesha kutunga kusanifu kutayarisha na pia kuimba nyimbo zake mwenyewe.
Image copyrightGettyImage captionPrince alitawala chati za muziki kote duniani katika miaka ya 70 na themanini
Vile vile aliwatungia nyimbo waimbaji wengi tu kote duniani.
Yamkini msanii huyo nguli alikuwa anaugua kwa kipindi kirefu na hata
alilazimika kukatiza Shoo zake kutokana na kudhohofika kwa afya yake.
0 maoni:
Chapisha Maoni