Shujaa Wetu,
Mwanahabari Mtoto, Mwanamazingira Balozi wa Umoja wa Mataifa UN kutoka Mwanza Tz, Getrude
Clement (16) jana amewasili nyumbani Jijini Mwanza majira ya saa tatu usiku na
kupokelewa kwa shangwe na ndugu, jamaa na marafiki katika Uwanja wa Ndege Mwanza.
Mwanahabari Mtoto, Mwanamazingira Balozi wa Umoja wa Mataifa UN kutoka Mwanza Tz, Getrude
Clement (16) jana amewasili nyumbani Jijini Mwanza majira ya saa tatu usiku na
kupokelewa kwa shangwe na ndugu, jamaa na marafiki katika Uwanja wa Ndege Mwanza.
Alihudhuria
Mkutano wa Umoja wa Mataifa nchini Marekani uliohusu Mabadiliko ya Tabia nchi
(Climate Change) ambapo alihutubia õakiwakilisha kundi la Watoto na Vijana
duniani.
Mkutano wa Umoja wa Mataifa nchini Marekani uliohusu Mabadiliko ya Tabia nchi
(Climate Change) ambapo alihutubia õakiwakilisha kundi la Watoto na Vijana
duniani.
Kutoka
Kushoto Pichani ni Brightius Titus ambae ni Katibu wa Mtandao wa Watoto
na Vijana Mkoani Mwanza MYCN, Katikati ni Getrude mmoja wa Watoto wa
Mtandao huo na Kulia ni Shaban Magana ambae ni Mwenyekiti wa MYCN.
"Kitu
ambacho nimejifunza ni kupata kujiamini zaidi kwa sababu ule Mkutano
ulihudhuriwa na watu wengi, wakiwepo viongozi kutoka zaidi ya nchi 170
wanachama wa Umoja wa Mataifa. Wameniasa kusoma zaidi ili kufikia
malengo yangu ambapo nitaendelea kuzungumza na wananchi pamoja na
viongozi wao juu ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo nitakuwa
balozi wao". Alisema Getrude.
"Wazazi wawaruhusu
watoto wao katika kushiriki shughuli mbalimbali za vikundi ili waweze
kujiamini zaidi katika kufikia ndoto zao". Anasema Mtoto Mwanahabari
Getrude.
Shabani
Njia (Kulia) ambae ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana na Watoto Mkoani
Mwanza MYCN akizungumzia mapokezi ya Mwanahabari na Balozi wa Mazingira
wa Umoja wa Mataifa akiwakilisha kundi la Watoto na Vijana Getrude
Clement
Clement Leon ambae ni baba mzazi wa Getrude akizungumzia mapokezi ya mwanae katika Uwanja wa ndege Mwanza.
Rizik Athman ambae ni mzazi wa Getrude
akizungumzia mapokezi ya mwanae katika Uwanja wa ndege Mwanza ambapo
anafurahishwa na hamasa aliyonayo mtoto wake ikiwemo kujiamini katika
masuala mbalimbali ikiwemo ya habari.
Getrude (Katikati) akiwa na Wazazi wake, Clement Leon (Kushoto) pamoja na Rizik Athman (Kulia).
Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Viongozi wa MYCN, mapema wakifurahia jambo wakati wakimsubiria Getrude
Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Viongozi wa MYCN wakiwa pamoja na Getrude.
Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na Viongozi wa MYCN, wakifurahia na Getrude katika picha ya pamoja.
Mapokezi ya Mtoto Getrude
Mapokezi ya Mtoto Getrude
Mapokezi ya Mtoto Getrude, Wengi walimsubiria kwa hamu kubwa.
Shuja, Mwanahabari Mtoto, Mwanamazingira Balozi wa UN Getrude Clement baada ya kuwasili Jijini Mwanza.
0 maoni:
Chapisha Maoni