Mwenyekiti wa Mfuko wa mchezo wa
Chess Tanzania (TCF) Bw. Vinay Choudary akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Ubingwa wa Afrika, Kanda ya
4.2 ya mchezo huo jana jijini Dar es Salaam. Kanda ya 4.2 inahusisha
nTimu kutoka nchi za Misri, Ethiopia, Eritria, Sudan, Sudani Kusini,
Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia,Djibouti na wenyeji
Tanzania.Mashindano hayo yameanza jana tarehe 23 April hadi April
31ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa
Chess Tanzania (TCA) Bw. Geofrey Mwanyika akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Ubingwa wa Afrika, Kanda ya
4.2 ya Mchezo huo jana jijini Dar es Salaam. Kanda ya 4.2 inahusisha
Timu kutoka nchi za Misri, Ethiopia, Eritria, Sudan, Sudani Kusini,
Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia,Djibouti na wenyeji Tanzania.
Rais wa Chama cha Mchezo wa Chess
Malawi, ambaye pia ni ni Mbunge mstaafu wa wa Bunge La nchi hiyo Mhe.
Kezzie Msukwa akizungumza namna Mhcezo huo Mchezo huo ulivyopiga hatua
nchini Tanzania ukilinganisha na kwao jana jijini Dar es Salaam wakati
wa ufunguzi wa Mashindano ya Ubingwa wa Afrika, Kanda ya 4.2 ya Mchezo
huo jana jijini Dar es Salaam. Kanda ya 4.2 inahusisha Timu kutoka nchi
za Misri, Ethiopia, Eritria, Sudan, Sudani Kusini, Kenya, Uganda,
Rwanda, Burundi, Somalia,Djibouti na wenyeji Tanzania. Mbunge huyo wa
zamani wa Malawi yupo nchini kama Mwamuzi katika mashindano hayo.
Baadhi ya washiriki wa Mashindano
ya Ubingwa wa Chess Afrika, Kanda ya 4.2 kimchezo huo wakiendelea
kuchuana jana jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yanendelea katika
Ukumbu uliopo Hotel ya Peackok ambapo mshindi katika mashindano hayo
atajinyakulia kitika cha Euro 3000.
Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya Ubingwa wa Chess Afrika, Kanda ya 4.2 kimchezo huo wakiendelea kuchuana jana jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yanendelea katika Ukumbu uliopo Hotel ya Peackok ambapo mshindi katika mashindano hayo atajinyakulia kitika cha Euro 3000.
0 maoni:
Chapisha Maoni