Rais
Barack Obama amesema anaunga mkono Uingereza kubaki katika jumuiya ya
umoja wa Ulaya ili kuweza kuchangia katika vita dhidi ya ugaidi na
masuala wahamiaji na utatuzi wa migogoro ya kiuchumi.RaisAmeyasema hayo
mwanzoni mwa ziara yake nchini humo.
Rais
Obama amekaririwa na gazeti la Uingereza Telegraph,akisema kwamba
uanachama wa Uingereza katika umoja wa Ulaya una umuhimu mkubwa na
endapo nchi hiyo itajiondoa katika umoja huo itapunguza nguvu katika
vita dhidi ya ugaidi duniani,suala la wahamiaji na utatuzi wa matatizo
ya kiuchumi.
Hata
hivyo Obama amesema anatete hoja ya umoja wa Ulaya kuendelea kama ulivyo
badala ya Uingereza kujitioa,japo kuwa anakabiliwa na upinzani kutoka
kwa viongozi wa juu wa Uingereza wanapiga kampeni kujitoa katika umoja
huo.
Naye meya
wa mji wa London Boris Johnson amesema Marekani isingeweza kuuza sehemu
ya demokrasia yake kama ambavyo Uingereza imefanya kwa umoja wa Ulaya.
Hii leo
Rais Obama anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Uingereza David
Cameroon kwa mazungumzo na baadaye chakula cha mchana na malkia
Elizabeth wa Uingereza hii ikiwa ni siku moja baada ya maadhimisho ya
miaka 90 ya kuzaliwa kwake.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni