Mkuu wa
wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza jambo na wataalamu
alioongozana nao katika uwanja mdogo wa ndege wa Moshi kwa ajili ya
kuruka na ndege ndo ya Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwa ajili ya
kujionea hali ya mafuriko.
Mkuu wa
wilaya akiwa katika uwanja wa ndege wa Moshi kwa ajili ya maandalizi ya
kwenda kujionea hali ya mafuriko katika maeneo mbalimbali.
Mtaalamau
anayeshughulikia Majanga kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Canon Masanja (wa tatu toka kulia) akimuelekeza jambo rubani muda mfupi
kabla ya ndege kuruka.
Mkuu wa
wilaya ya Moshi akiteta jambo na Kaimu meneja wa uwanja mdogo wa ndege
wa Moshi ,Fredrick Kimaro muda mfupi kabla ya kwenda kutizama eneo
lililo athirika kwa mafuriko.
Maeneo
mbalimbali ,zikiwemo nyumba zikiwa zimezingirwa na maji katika vijiji
vya Miwaleni huku mashamba yakiwa yameharbika vibaya.
Mioundo mbinu ya barabara pia imeathirika vibaya.
Maashamba yamejaa maji.
Maeneo
mengine barabara hazipitiki hali inayochangia wananchi wanaoishi katika
maeneo hayo kushindwa kupata huduma za kibinadamu.
Eneo la Mabogini pia liliathirika na mafuriko ingawa yalikuwa ni ya muda mfupi.
Sehemu ya mji wa Moshi unavyoonekana kwa juu.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
0 maoni:
Chapisha Maoni