KATIKA Kuhakikisha Wananchi Wanaepukana
na Vimelea Vya Magonjwa yatokanayo na chakula Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA) imeishauri jamii kuongeza umakini katikakuandaa vyakula Vya kwenye mighahawa ila
kuhakikisha vyakula hivyo vinavyopikwa vinakuwa salama kwa ajili ya afya ya
mlaji ili kuepukana na magonjwa yatokananyo na kula vyakula ambacho sio salama ikiwa
ni sehemu ya mkakati wao wa kuepukana na magonjwa.
Kauli hiyo
imetolewa Mwishoni Mwa w iki na Meneja wa Uchanganuzi wa madhara yatokananyo na
chakula na dawa TFDA Makao makuu Kandida Shirima.
Kandida alisema kuwa tatizo la watu kula vyakula
ambavyo sio salama ni kubwa hali ambayo
imeilazimu serikali kutoa elimu juu ya madhara yatokanayo na kula vyakula
ambavyo si salama kwa afya zao(chakula kichafu).
Pia alisema kuwa
wameamua kuweka mfumo huo ili kutambua magonjwa yanayotokea nchini ambayo
yanatokana na kula chakula kichafu.
Naye Ofisa Afya wa Mkoa wa Njombe Mathias Gambishi ambaye
alizungumzia suala la magonjwa yatokanayo na kula chakula kisicho salama
alisema kuwa hali ya watu kuugua magonjwa kwenye mkoa wake hayana tofauti na mikoa mingine kwani
magonjwa wanayougua ni kama kuumwa homa ya matumbo,kuhara ama kipindupindu.
Gambishi alisema kuwa inakadiriwa watu Milioni
600 huugua duniani kwa Mwaka kwa kula chakula kisicho salama huku watu 420,000
hupoteza maisha
0 maoni:
Chapisha Maoni