Mkuu
wa Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa Tigo, David Zacharia
(kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es
Salaam leo asubuhi kuhusu huduma iliyoanzishwa na kampuni hiyo ya
kutiririsha video za YouTube bure ambayo itakuwa inapatikana kwa
wateja wote wa Tigo kuanzia saa 6.00 usiku hadi saa 12.00 alfajiri.
Kulia ni Meneja Mawailiano wa Tigo, John Wanyancha.
Meneja Mawailiano wa Tigo, John Wanyancha (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
………………………………………………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
Kampuni
inayoongoza kwa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania imetangaza
upatikanaji wa huduma ya bure ya kutiririsha video za YouTube nyakati za
usiku kwa watumiaji wake wote ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya
simu kutoa huduma hiyo kwenye mitandao ya kijamii bila tozo hapa
nchini.
Akitangaza
tukio hilo jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya
Mawasiliano wa Tigo, David Zacharia aliviambia vyombo vya habari kuwa
huduma ya kutiririsha video za YouTube bure itakuwa inapatikana kwa
wateja wote wa Tigo kuanzia saa 6.00 usiku hadi saa 12.00 alfajiri.
Tigo ina wateja zaidi ya milioni 10. Ikiwa
imezinduliwa Mei 2005, YouTube ni utiririshaji wa video ambao
uunatumiwa na wafuasi zaidi ya bilioni 1 duniani kote, takribani
theluthi moja yake wakiwa wanatumia intaneti.
Huduma
hiyo inawapa fursa ya kuangalia video za YouTube kwa muda wa saa nyingi
yakiwawo pia mabilioni ya maoni. Aidha inaruhusu mabilioni ya watu
kugundua, kuangalia na kushirikiana video ambazo awali zilibuniwa na
kubuni jukwaa na kuunganisha, kuhabarisha na kuvutia wengine sehemu
mbalimbali duniani.
“Kitu
pekee kinachohitajika ili kuweza kupata data za bure katika kutiririsha
video za YouTube ni kuwa na aina ya simu itakachoweza data hizo.
Tunaamini huduma hii mpya itaendelea kuonesha kujituma kwetu kwenye
kuboresha mabadiliko kwenye maisha ya kidijitali na kuongoza kutoa
teknolojia ya hali ya juu pamoja na ubinifu kwa wateja wetu,” alisema
Zacharia.
Pamoja
na utriririshaji huo watumiaji wa YouTube pia wateja watakuwa na njia
mbadala ya kuweka video kwenye simu zao ambayo ni programu ya simu
inayojulikana kama YouTube Offline inayomwezesha mtumiaji kuongeza
video kwenye simu yake ili aweze kuiangalia baadaye wakati ambapo
muunganisho na itaneti unakuwa haupo au upo chini.
Kwa
video ambazo pale ambapo zinapatikana watumiaji wanaweza kuchagua
kuongeza video kwa kuzitiririsha na kwa ajili ya kuangalia hapo
baadaye kwa kutumia kitufe cha ‘offline’.
Ikiwa
imeshachukuliwa kwa njia hiyo video hiyo inaweza kuchezeshwa bila
kuunganishwa na intaneti kwa muda wa hadi saa 48, hivyo mtumiaji anaweza
kuzifurahia video zake za YouTube bila hofu ya maunganisho na intaneti
kuwa yapo chini.
Zacharia
aliongeza kwamba kuzifikia data bure kutakuwa kunapatikana kwa
wateja wa Tigo wa huduma ya malipo kabla bila kuwepo malipo maalum
yanayohitajika kuifurahia huduma hiyo.
Upatikanaji
bure wa data za huduma ya kutiririsha video za YouTube umefanyika baada
ya kampuni hiyo ya simu kutangaza huduma nyingine ya bure ya WhatsApps
kwa wateja wake mwanzoni mwa mwaka huu ambako pia kulitamnguliwa na
kiuzinduliwa kwa huduma ya Facebook ya Kiswahili mwaka 2014.
Tigo
inayofuraha kujumuisha majkuwaa ya video kwenye ofa hii. Kama wewe ni
msambazaji wa huduma ya video unaweza kuwasiliana nasi kupitia
customercare@tigo.co.tz
0 maoni:
Chapisha Maoni