Bw.
James Oigo Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii NSSF akizungumza na waandhishi wa habari katika makao makuu ya
shirika hilo jengo la Benjamin Mkapa wakati akielezea kuhusu waajiri
wanaodaiwa madeni sugu ya michango ya wafanyakazi wao na kutamka kwamba
wasipolipa michango hiyo mpaka ifikapo Juni 30 mwaka huu shirika hilo
linawapeleka mahakamani, kulia ni mmoja wa maofisa waandamizi wa shirika
hilo Bw. Salim Khalifan pamoja na maofisa wengine wa shirika hilo
waliohudhuria katika mkutano huo.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa hiyo wakati Bw James Oigo
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
NSSF akizungumza nao katika mkutano huo.
………………………………………………………………………………………………………………………
Shirika la Taifa la Hifadhi ya
jamii (NSSF) linapenda kutoa wito kwa waajiri wote wanaodaiwa
malimbikizo ya michango ya wafanyakazi wao kulipa malimbikizo hayo kabla
ya tarehe 30.06.2016.
Waajiri ni moja kati ya wadau
wakubwa wa shirika letu la NSSF kwa mujibu wa kifungu cha 11(6) na 12
(1) cha sheria ya NSSF, waajiriwa wana majukumu makubwa mawili.
- Kuhakikisha wafanyakazi wao wanaandikishwa katika shirika la taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) mara tu wanapoajiriwa.
- Kuwakata michango yao asilimia 5% au 10% kutoka kwenye mshahara wa mwezi na kuwasilisha mchango huo ukiwa ni asilimia 20% ya mshahara wa mwezi, maana yake ni kwamba mwajiri baada ya kufanya makato kutoka katika mshahara wa mfanyakazi wake, anatakiwa kuongeza asilimia 10% au 15% ili ifikie asilimia 20% na kuwasilisha kwenye shirika.
Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha
sheria ya NSSF no 28 ya mwaka 1997, waajiri wote wanatakiwa wawasilishe
michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku 30 toka tarehe ya mwisho wa
mwezi husika, kwa mfano mchango wa mwezi machi,2016 , unatakiwa uwe
umewasilishwa kwenye shirika kabla ya tarehe 30/4/2016 kinyume na hapo
ni ukiukwaji wa sheria na ni kosa la jinai.
Lakini kuna baadhi ya waajiri kwa
sababu wanazozijua wenyewe, wanashindwa kutekeleza hitaji hili la
kisheria kikamilifu kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi
wao kwa wakati.
Kitendo cha kutowasilisha
michango ya wafanyakazi wao kwa wakati si tu kwamba ni kosa la jinai
kwa mujibu wa kifungu cha 72 (d) cha sheria ya NSSF na ambayo adhabu
yake ni pamoja na kifungo cha miaka 2 jela, lakini pia ucheleweshaji huu
unasababisha madhara makubwa kwa wanachama na shirika kwa ujumla.
Kutowasilisha michango kwa wakati
husababisha usumbufu mkubwa kwa wanachama pale wanapostaafu kazi na
kutakiwa kulipwa mafao yao ya uzeeni, hali hii husababisha wanachama
kucheleweshewa malipo yao kwa makosa ambayo si ya kwao. Na wakati
mwingine shirika hulazimika kuwalipa wanachama hawa kwa hasara kwa
sababu waajiri wameshindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi husika.
Ili kuendana na kasi ya Mh. Rais
John Pombe Magufuli na “motto” wake wa “Hapa kazi tu” shirika limeandaa
mpango mkakati wa kuwapitia / kuwatembelea waajiri wote katika jiji la
dsm na mikoa yote tanzania bara ambao wanadaiwa michango ya wafanyakazi
wao ili kuweza kukusanya michango hiyo . Mpango huu wa kuwatembelea
waajiri hawa itaanza rasmi tarehe 2/5/2016. Maafisa wa shirika
watawapitia waajiri hawa mmoja baada ya mwingine na hakuna hata mmoja
atakayeachwa bila kutembelewa alimradi anadaiwa michango ya
wafanayakazi.
Kumbukumbu tulizonazo, kwa mfano
katika jiji la Dar es salaam pekee mpaka mwezi machi, 2016 waajiri
wapato 3,234 wanadaiwa kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao wenye
jumla ya shs milioni 21,497.35 hali hii haiweze kuvumilika hata kidogo
na ni kinyume kabisa na mwenendo kasi wa mh. Rais magufuli katika
kukwaletea watanzania maendeleo endelevu na motto wake wa hapa kazi tu.
Shirika linatoa wito kwa waajiri
wote kuhakikisha wanalipa michango ya NSSF ya wafanyakazi wao kwa wakati
na linawataka waajiri wanaodaiwa kuhakikisha wanalipa malimbikizo yote
ifikapo tarehe 30.06.2016 pia tunawaomba waajiri wote wanaodaiwa watoe
ushirikiano kwa maafisa wetu pale watakapowatembelea katika maeneo yao
ya kazi ili kufikia muafaka wa pamoja wa jinsi ya kulipa madeni haya
ndani ya muda uliowekwa yaani tarehe 30.06.2016.
Itakapofika mwezi julai, 2016
shirika halitakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kuwapeleka
mahakamani waajiri wote wanaodaiwa michango ya wafanyakazim, tungependa
kila mwajiri atomize wajibu wake ili kuepuka usumbufu wa muda na mambo
mengine lengo la nssf siku zote ni kuwa na mahusiano mazuri na waajiri
na hatua za kisheria dhidi ya waajiri zinachukuliwa kama hatua za mwisho
(Last resort) za kumfanya mwajiri atomize wajibu wake pale ambapo njia
zingine zote zimeshindikana (zimegonga mwamba), lakini katika mazingira
ya kawaida shirika halitarajii kwamba waajiri watashidnwa kutimiza
wajibu wao mpaka wachukuliwe hatua za kisheria. Aidha kwa upande
mwingine, serikali pamoja na vyombo vya sheria, mahakama na ofisi ya
mwendesha mashitaka mkuu wa serikali (DPP) wameahidi kutoa ushirikiano
kwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii – NSSF katika kutekeleza
majukumu yake.
Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF) linapenda kutoa wito kwa waajiri wote wanaodaiwa
malimbikizo ya michango ya wafanyakazi wao kulipa malimbikizo hayo kabla
ya tarehe 30.06.2016.
Waajiri ni moja kati ya wadau
wakubwa wa shirika letu la NSSF kwa mujibu wa kifungu cha 11(6) na 12
(1) cha sheria ya nssf, waajiriwa wana majukumu makubwa mawili.
- Kuhakikisha wafanyakazi wao wanaandikishwa katika shirika la taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) mara tu wanapoajiriwa.
- Kuwakata michango yao asilimia 5% au 10% kutoka kwenye mshahara wa mwezi na kuwasilisha mchango huo ukiwa ni asilimia 20% ya mshahara wa mwezi, maana yake ni kwamba mwajiri baada ya kufanya makato kutoka katika mshahara wa mfanyakazi wake, anatakiwa kuongeza asilimia 10% au 15% ili ifikie asilimia 20% na kuwasilisha kwenye shirika.
Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha
sheria ya nssf no 28 ya mwaka 1997, waajiri wote wanatakiwa wawasilishe
michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku 30 toka tarehe ya mwisho wa
mwezi husika, kwa mfano mchango wa mwezi machi,2016 , unatakiwa uwe
umewasilishwa kwenye shirika kabla ya tarehe 30/4/2016 kinyume na hapo
ni ukiukwaji wa sheria na ni kosa la jinai.
Lakini kuna baadhi ya waajiri kwa
sababu wanazozijua wenyewe, wanashindwa kutekeleza hitaji hili la
kisheria kikamilifu kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi
wao kwa wakati.
Kitendo cha kutowasilisha
michango ya wafanyakazi wao kwa wakati si tu kwamba ni kosa la jinai
kwa mujibu wa kifungu cha 72 (d) cha sheria ya nssf na ambayo adhabu
yake ni pamoja na kifungo cha miaka 2 jela, lakini pia ucheleweshaji huu
unasababisha madhara makubwa kwa wanachama na shirika kwa ujumla.
Kutowasilisha michango kwa wakati
husababisha usumbufu mkubwa kwa wanachama pale wanapostaafu kazi na
kutakiwa kulipwa mafao yao ya uzeeni, hali hii husababisha wanachama
kucheleweshewa malipo yao kwa makosa ambayo si ya kwao. Na wakati
mwingine shirika hulazimika kuwalipa wanachama hawa kwa hasara kwa
sababu waajiri wameshindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi husika.
Ili kuendana na kasi ya mh. Rais
Dk. John Pombe Magufuli na “Motto” wake wa “hapa kazi tu” shirika
limeandaa mpango mkakati wa kuwapitia / kuwatembelea waajiri wote katika
jiji la dsm na mikoa yote tanzania bara ambao wanadaiwa michango ya
wafanyakazi wao ili kuweza kukusanya michango hiyo . Mpango huu wa
kuwatembelea waajiri hawa itaanza rasmi tarehe 2/5/2016. Maafisa wa
shirika watawapitia waajiri hawa mmoja baada ya mwingine na hakuna hata
mmoja atakayeachwa bila kutembelewa alimradi anadaiwa michango ya
wafanayakazi.
Kumbukumbu tulizonazo, kwa mfano
katika jiji la Dar es salaam pekee mpaka mwezi machi, 2016 waajiri
wapato 3,234 wanadaiwa kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao wenye
jumla ya shs. milioni 21,497.35 hali hii haiweze kuvumilika hata kidogo
na ni kinyume kabisa na mwenendo kasi wa mh. Rais magufuli katika
kukwaletea watanzania maendeleo endelevu na motto wake wa hapa kazi tu.
Shirika linatoa wito kwa waajiri
wote kuhakikisha wanalipa michango ya NSSF ya wafanyakazi wao kwa wakati
na linawataka waajiri wanaodaiwa kuhakikisha wanalipa malimbikizo yote
ifikapo tarehe 30.06.2016 pia tunawaomba waajiri wote wanaodaiwa watoe
ushirikiano kwa maafisa wetu pale watakapowatembelea katika maeneo yao
ya kazi ili kufikia muafaka wa pamoja wa jinsi ya kulipa madeni haya
ndani ya muda uliowekwa yaani tarehe 30.06.2016.
Itakapofika mwezi julai, 2016
shirika halitakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kuwapeleka
mahakamani waajiri wote wanaodaiwa michango ya wafanyakazim, tungependa
kila mwajiri atomize wajibu wake ili kuepuka usumbufu wa muda na mambo
mengine lengo la NSSF siku zote ni kuwa na mahusiano mazuri na waajiri
na hatua za kisheria dhidi ya waajiri zinachukuliwa kama hatua za mwisho
(Last resort) za kumfanya mwajiri atomize wajibu wake pale ambapo njia
zingine zote zimeshindikana (zimegonga mwamba), lakini katika mazingira
ya kawaida shirika halitarajii kwamba waajiri watashidnwa kutimiza
wajibu wao mpaka wachukuliwe hatua za kisheria. Aidha kwa upande
mwingine, serikali pamoja na vyombo vya sheria, mahakama na ofisi ya
mwendesha mashitaka mkuu wa serikali (DPP) wameahidi kutoa ushirikiano
kwa hsirika la taifa la hifadhi ya jamii – NSSF katika kutekeleza
majukumu yake.
0 maoni:
Chapisha Maoni