Mshambuliaji
Ramadhani Madebe wa Uchukuzi SC akikokota mpira katikati ya uwanja,
huku Mohamed Salum wa GGM akimsogelea. Timu hizo zimetoka satre ya bao
1-1.
Issack Ibrahim (mwenye mpira) akimtoa Fernand Makanga wa GGM akimzuia asilete madhara. Timu zilitoka sare 1-1.
Mshambuliaji
Oswald Binamungu wa GGM akitafuta mbinu za kumtoka Ally Poloto wa
Uchukuzi SC. Timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
Ramadhani Mwalongo wa Uchukuzi akimalizia mbio za marathoni kwa wanaume na kuibuka mshindi wa tatu kwa kutumia muda wa 0.48:17.
Mayasa
Hamidu (C) wa Uchukuzi SC akiangalia wa kumrushia mpira huku Nathereth
Mwanjala (WA) wa Tanesco akisogea kumuwahi . Uchukuzi aliibuka washindi
kwa magoli 31-13.
Prisca Ferdinand wa Uchukuzi SC (kulia) akilamba karata mbele ya
mpinzani wake Theodora Stanslaus wa Ujenzi katika mashindano ya Mei
Mosi.
…………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu Dodoma
TIMU
za mchezo wa netiboli za CDA Dodoma na Uchukuzi SC jana ziliendeleza
ubabe kwa kuwafunga wapinzani wao bila huruma kwenye mashindano ya Mei
Mosi yanayoendelea kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
CDA
Dodoma inayoundwa na wachezaji wazoefu iliwafunga TPDC kwa magoli 38-12.
Washindi walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 21-6.
Nao
wadada machachari wa Uchukuzi SC wakiongozwa na kocha wao maarufu,
Judith Ilunda waliwafunga Tanesco kwa magoli 31-13. Hadi mapumziko
washindi walikuwa mbele kwa magoli 19-5.
Wafungaji
mahiri wa Uchukuzi SC, Matalena Mhagama alipachika magoli 17 na Grace
Mwasote magoli 14, huku Caltace Monampo wa Tanesco alifunga matano na
mwenzake Sandra Mfaume magoli nane.
Katika
mchezo wa soka, timu ya Uchukuzi SC iliwahenyesha Geita Gold Mine (GGM)
na kutoka sare ya bao 1-1. GGM ndio walioanza kupata bao dakika ya 33
kwa mshambuliaji wake Oswald Binamungu aliunganisha krosi ya Quentin
George, na Ramadhani Madebe aliyekuwa akihaha uwanja mzima kusaka bao
aliisawazishia Uchukuzi katika dakika za nyongeza.
Katika
mchezo mwingine wa soka, timu ya Ukaguzi waliwachapa wenyeji CDA kwa
magoli 4-1. Victor Ngalawa ndio alikuwa wa kwanza kuandika bao katika
dakika ya sita, na Pemsi Msenga alisawazisha katika dakika ya 18.
Ukaguzi
waliendelea kuwashambulia CDA na Deo Masanja (mchezaji wa zamani wa
Simba SC) aliongeza bao la pili katika dakika ya 33, huku Ally Mpondo
alifunga la tatu dakika ya 82 na Yahya Salum alifungala nne dakika ya
89.
Katika
mchezo wa riadha mbio za marathoni wanaume ameshinda Atson Mbughuni wa
Tamisemi kamaliza kwa 0:35.32, wapili ni Lazaro Lugano wa tanesco
katumia 0:42.45 na watatu ni Ramadhani Wakilongo wa Uchukuzi SC katumia
0:48.17.
Upande
wa wanawake riadha alishinda Stella Mroso wa TPDC kwa 0:42.36, huku wa
pili ni Beltila Genadius wa Tamisemi kwa 0:44.00 na watatu ni
Scholastica Halisi wa Uchukuzi kwa 0:49:21.
Katika
michezo ya jadi kwa upande wa karata wanawake bingwa ni Sheila Mwihava
wa Tanesco alimshinda Mayasa Kambi wa UDOM katika fainali na mshindi wa
tatu ni Bupe Munisi wa Mawasiliano, kwa upande wa wanaume ametwaa
ubingwa Haji Chilo wa UDOM, huku wa pili ni Omari Said wa Tanesco na
watatu ni Ally Zongo wa Uchukuzi SC
0 maoni:
Chapisha Maoni