SHUKURU KAWAMBWA AMWAGA MIFUKO YA SARUJI
Katibu wa mbunge wa
jimbo la Bagamoyo, Magreth Masenga kushoto akikabidhi mifuko ya saruji
tani moja juzi kwa kwani mkuu msaidizi katika shule ya Msingi Kizuiani
Nurdin Napunda wa katikati .(picha na Mwamvua Mwinyi)
…………………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MBUNGE wa jimbo la
Bagamoyo mkoani Pwani, dk Shukuru Kawambwa, ametoa tani Tatu za mifuko
ya saruji katika shule ya msingi Kizuiani, shule ya awali ya Mtoni na
zahanati ya Nianjema ambapo kila sehemu imekabidhiwa tani moja moja.
Mbunge huyo ametoa
mifuko hiyo kwa lengo la kutimiza ahadi yake aliyoitoa mwezi feb mwaka
huu alipofanya ziara ya kutembelea shule na zahanati mbalimbali jimboni
humo.
Aidha amepeleka mafuta ya dizeli Lita 200 yatakayosaidia kutumika katika gari la shule ya sekondari fukayose.
Akikabidhi tani hizo
juzi,katibu wa mbunge wa jimbo la Bagamoyo ,Magreth Masenga ,alisema
walipotembelea shule ya Kizuiani walikuta walimu wa shule hiyo hawana
matundu ya vyoo hali inayosababisha kujisaidia kwa mwalimu anaishi
jirani na shule
Alieleza kuwa baada ya
kujionea hali hiyo isiyoridhisha mbunge huyo aliona kuna kila sababu ya
kuwezesha saruji ili kusaidia kuanza kwa ujenzi kwa kushirikiana na
wadau na jamii kijumla.
Magreth alisema shule
ya awali ya Mtoni aliahidi kuwaunga mkono wananchi ambao walishaanza
ujenzi wa darasa la awali na lengo lao kubwa ni ianze mwaka huu.
Alisema katika zahanati
ya Nianjema amepeleka tani moja kwa lengo la kusaidia ujenzi wa
zahanati hiyo ambayo wakazi wa eneo hilo walianza kuijenga kwa nguvu zao
,zahanati itakayowasaidia kuwaondolea adha ya kufuata huduma ya afya
mbali.
“Alipita kwenye shule
hizo na zahanati ya Nianjema na kote amepeleka tani moja moja ,si kwamba
atakuwa amemaliza changamoto zao lakini itakuwa imesaidia kuendeleza
pale palipobakia ” alisema Magreth kwa niaba ya dk.Kawambwa.
Magreth alisema shule ya sekondari fukayose mbunge alikuwa tatizo la usafiri katika shule hiyo ambayo ipo mbali na mji.
Alieleza kuwa gari
lililopo shuleni hapo lilitolewa na shirika la Goodneighbours shirika
ambalo limejenga shule hiyo lakini tatizo lilikuwa ni mafuta kwasasa .
Akizungumza changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu jimbo hapo alisema ni
miundombinu kuwa chakavu kwenye baadhi ya shule,uhaba wa matundu ya vyoo
na madarasa na upungufu wa walimu na madawati.
Nae mwalimu mkuu
msaidizi katika shule ya msingi Kizuiani Nurdin Napunda ,alimshukuru dk
Shukuru Kawambwa kwa ahadi anazotoa kwa wakati.
Napunda alisema mbunge huyo alishawahi kuwasaidiaa computer mpakato kumi na ceiling board .
Shule ya msingi
Kizuiani bado inakabiliwa na upungufu wa madawa ni 421 na madarasa 19
,upungufu uliosababishwa na ongezeko wanafunzi wa darasa la kwanza
walioandikishwa mwaka 2016.
0 maoni:
Chapisha Maoni