Daladala
zinazofanya safari zake katikati ya jiji zimetakiwa kuondoka ifikapo
Mei 2 Mwaka huu ilikupisha mradi wa mabasi yaendayo kasi kuweza kufanya
shughuli zake kuanzia hiyo Mei 10.
Kwa
mujibu wa Msemaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (Dart), ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar es Salaam
(Darcoboa), Sabri Mabrouk amebainisha kuwa, tayari wamiliki wote wa
mabasi walishalipwa fidia ya kubadili njia.
“Wamiliki
wote wa mabasi wameshalipwa fedha zao tangu Desemba mwaka jana, hakuna
anayedai na tumewapa siku saba kuondoka barabara kabla ya Mei 10,”
amesema Mabrouk.
Mradi
wa Dart unatarajia kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu na tayari mabasi hayo
yameshaanza kufanya majaribio katika njia mbali mbali katikati ya jiji
huku changamoto kubwa ikidaiwa na waendesha pikipiki, raia na daladala
kupita kwenye njia hiyo ya mradi na kusababisha msongamano wa magari
kitendo ambacho kinalazimu mabasi hayo nayo kujikuta yakikaa folenI.
Aidha waweza kujionea hapa taarifa za utaratibu wa mabasi hayo:
Mabasi yataanza saa 12 kasoro robo kutokea Depot ya Jangwani kwa mpangilio huu wa hapa chini:
- RUTI YA KIMARA- KIVUKONI Mabasi Sita (6). Kati ya mabasi Hayo sita wakati wa Kutoka Jangwani matatu yataenda Kimara na Matatu Kivukoni.
- RUTI YA KIMARA – KARIAKOO Mabasi Sita (6). Kati ya hayo Matatu yataelekea Kariakoo na Matatu Kimara.
- RUTI YA UBUNGO – KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi Manne yataelekea Ubungo na Manne Kivukoni.
- RUTI YA UBUNGO – KARIAKOO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Mabasi manne Yataenda Ubungo na Manne yataenda Kariakoo.
- RUTI YA UBUNGO – MOROCCO Mabasi nane (8). Kati ya hayo Manne yataenda Ubungo Manne yataenda Morocco.
- RUTI YA MOROCCO – KARIAKOO Mabasi sita (6). Kati ya hayo mabasi Matatu Morocco na Matatu Kariakoo.
- RUTI YA MOROCCO – KIVUKONI Mabasi nane (8). Kati ya Hayo Mabasi Manne yataenda Moroco na mabasi manne Kivukoni.
DESPATCH PLAN SAA KUMI NA MBILI KAMILI.
- Kimara Terminal Mabasi Sita (6)
- Ubungo Terminal Mabasi kumi na mbili (12)
- Morocco Termial Mabasi kumi na moja (11)
- Kariakoo Terminal Mabasi kumi (10)
- Kivukoni Terminal Mabasi kumi na moja (11)
JUMLA.NI MABASI HAMSINI (50)
mabasi hayo yakiwa katika majaribio..
0 maoni:
Chapisha Maoni