Wanasheria Mblaimbali kutoka Kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake nchini Tanzania WLAC wakiwa nje ya mahakama kuu ya Tanzania Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufungua Jalada la kesi hiyo ambayo inatajwa kuwasaidia wanawake wajane nchini |
Na Exaud Mtei
Kufuatia changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo
wanawake wajane nchini hasa baada ya kufiwa na wenza wao kituo cha msaada wa
kisheria kwa wanawake nchini Tanzania WLAC kimeamua kufungua kesi mkakati
katika mahakama kuu ya Tanzania kesi yenye lengo la kutetea haki ya mjane
kupata mchango wake katika mali zilizopatikana kwa pamoja wakati wa ndoa.
Hatua hiyo imekuja baada ya kujengeka mazoea kuwa mara
baada ya kufariki kwa mwanaume katika ndoa mali zote zimekuwa zikihesabika kuwa
ni za mwanaume na kusahau mchago wa mwanamke wakati wa utafutaji wa mali hizo
jambo ambalo limepelekea shirika hilo kuitaka mahakama kuweka wazi juu ya swala
hilo ili kuwasaidia wajane hao.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa jalada la kesi hiyo katika mahakama kuu ya
Tanzania wakili wa kujitegemea ambaye ndiye anayesimamia kesi hiyo
wakili Alphonce Katemi amesema kuwa hali hiyo imekua inakiuka katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofayiwa
mabadiliko mara kwa mara ambayo inatambua usawa wa binadamu,haki sawa
mbele ya sheria,na haki ya kumiliki mali na hifadhi ya mali hiyo kwa
mujibu wa sheria.
Amesema
kuwa kutokana na hilo WLAC imeamua kufungua keshi mkakati(starategic
litigation case) kesi namba 10 kuomba Tamko la mahakama kutambua haki ya
mjane kupata mchango wake katika mali zilizopatikana kwa pamoja wakati
wa ndoa pale anapofiwa na mume wake kabla mali hizo hazijaingizwa kwenye
mirathi na kugawanywa kwa warithi wengine wa marehemu jambo ambalo
wamesema litasaidia kupata haki ya jasho lao kama ambavyo sheria ya ndoa
ya mwaka 1971 inatambua wakati wa talaka au kutengana kwa wanandoa
Wakili wa kujitegemea Alphonce Katemi ambaye ndiye anayesimamia kesi hiyo akizngumza na wanahabari nje ya mahakama kuu tanzania kuhusu lengo hasa la kesi hiyo na kwanini wameamua kufungua kesi ya aina hiyo kutaka ufafanuzi wa mahakama |
wanasheria pomoja na mawakili ambao ndio wamefungua jalada hilo wakiwa wanazungumza na wanahabari Ndani ya mahakama hiyo mapema leo |
Baadhi ya wanawake waliofika kushughudia tukio hilo wakizungumza na wahabari kuhusu hali inayowakumba wajane baada ya kufiwa na wenza wao ambao kina mama hao wameonyeshaa kufurahishwa kwao kwa kufunguliwa kwa jadala hilo ambalo wamesema linaweza kuwaokoa wajane nchini Tanzania kama mahakama itaweka wazi na kuwapa haki sawa wajane nchini |
0 maoni:
Chapisha Maoni