Mbunge wa jimbo la
Chalinze mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete alipokwenda jana kutembelea
shule ya sekondari Chalinze baada ya bweni la wanafunzi wa kiume kuungua
kutokana na shoti ya umeme. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
……………………………………………………………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
WANAFUNZI 65 wa shule
ya sekondari chalinz e iliyopo Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
wamenusurika kifo baada ya bweni lao kuteketea kwa moto wakati wao
wakiwa darasani kwa ajili ya kujisomea masomo ya usiku.
Akizungumza na
MWANDISHI WA HABARI HIZI kwa njia ya simu mkuu wa wilaya ya Bagamoyo
Majid Mwanga alisema tukio hilo limetokea april 17 majira ya saa 3:20
usiku .
Mkuu huyo alisema
chanzo cha moto huo inadaiwa ni shoti ya umeme ambayo imesababisha moto
huo kuteketeza vifaa vyote vikiwemo magodoro,vitanda,vitabu katika bweni
hilo.
Mwanga akizungumzia
kuhusiana na juhudi za serikali ambazo tayari wameshazichukua hadi sasa
alisema wanawahifadhi wanafunzi hao katika jengo lingine la muda ambalo
lilikuwa linatumika kwa chakula.
Alisema kuwa pia serikali ya mkoa
imeshaanza kuwasiliana na wadau mbalimbali ambao watasaidia kununua
vifaa vya ujenzi kwa kusaidiana na serikali ili kujenga bweni jingine.
“Siwezi kusema hali ni nzuri
kutokana na watoto wameunguliwa vifaa vyao,ni hasara katika jengo pia
kwahyo kilichopo sasa ni kumshukuru mungu kwa wanafunzi hawa
kunusurika”alisema Mwanga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo Chalinze Hussein Mramba alikiri kutokea kwa tukio hilo
Alisema mkandarasi wa halmashauri ya wilaya hiyo bado anaendelea na tathmini ya miundombinu iliyoungua.
Shule ya sekondari Chalinze ina
jumla ya idadi ya wanafunzi 1,151 kati yao 65 kwa sasa wameunguliwa na
vitu vyao vyote hivyo kunahitajika juhudi za jamii,wadau na serikali
katika kuhakikisha wanatoa msaada wa hali na mali .
0 maoni:
Chapisha Maoni