Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni alipowasili
katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony John Mtaka
(kushoto) jana wakati wa ziara yake mkoani hapo kukutana na wadau wa
sekta anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa
mkoa huo.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu
Bibi. Mwamvua Jilumbi (aliyesimama) akitoa taarifa ya Mkoa wa Simiyu
upande wa sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa waziri mwenye
dhamana na sekta hizo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) alipofanya ziara jana
mkoani hapo kujua hali ya sekta hizo pamoja na kutoa vitendea kazi kwa
maafisa habari wa mkoa huo. Wapilikushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.
Anthony John Mtaka
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano
(TCRA) Kanda ya ziwa Eng. Lawi Odiero (aliyesimama) akijibu hoja wakati
wa ziara ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Nnauye kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia jana Mkoani Simiyu.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akikagua iPad kabla ya kumkabidhi
afisa habari wa Mkoa wa Simiyu Bibi. Stella Kalinga (kulia) wakati wa
ziara yake mkoani humo kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia jana
Mkoani Simiyu.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akizungumza na waandishi wa
Mkoa wa Simiyu baada ya kufanya ziara yake jana mkoani humo kwa kukutana
na wadau wa sekta anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa
maafisa habari wa mkoa huo.
Kaimu katibu msaidizi CCM Mkoa wa
Simiyu Bw. Gelison Nyamwihula akitoa taarifa ya chama mkoani simiyu kwa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye
(katikati) alipotembelea ofisi za CCM jana mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony John Mtaka
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo, Simiyu
………………………………………………………………………………………
Na: Genofeva Matemu – Maelezo, Simiyu
Vyombo vya habari nchini
vimetakiwa kuandaa vipindi vya kuelimisha na kupunguza burudani kwa
kuongeza idadi ya vipindi vya kujenga uzalendo, amani, mshikamano pamoja
na umoja wa kitaifa
Rai hiyo imetolewa na Meneja wa
Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Ziwa Eng. Lawi Odieri wakati wa
ziara ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye
alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia jana Mkoani Simiyu.
“Mamlaka ya mawasiliano
inafuatilia kwa karibu maudhui ya vyombo vya habari ili kuepusha maudhui
potofu na hatarishi yatakayoweza kuondoa mshikamano na uzalendo tulio
nao” alisema Eng. Odieri
Aidha Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA)
kutoa uwepo wa masafa ya kuanzishia vituo vya utangazaji katika Mkoa wa
Simiyu pamoja na mikoa mingine ya jirani ili kuweza kuongeza idadi ya
vituo vya utangazaji ambapo kwa mkoa wa Simiyu hadi sasa kuna kituo
kimoja tu cha utangazaji.
Mhe. Nauye amesema kuwa uwepo wa
vituo vya kutosha vya utangazaji katika mkoa wa Simiyu vitasaidia
kutangaza vivutio vya utalii wa kiutamaduni vilivyopo mkoani Simiyu
pamoja na kuinua wasanii wa mkoa huo kwa kuwapatia nafasi ya kurusha
nyimbo zao katika vituo hivo.
Mpaka sasa idadi ya vituo vya
redio nchini zenye leseni imeongezeka na kufikia vituo 123, wakati idadi
ya vituo vya televisheni zenye leseni katika mfumo wa dijitali nchini
umefikia 26 huku kanda ya ziwa ikiwa na jumla ya vituo vya redio 23 na
kituo kimoja cha televisheni.






0 maoni:
Chapisha Maoni