Shirkisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), limelaani kitendo cha baadhi ya mashabiki wa mpira wa
miguu kufanya vurugu mara baada ya mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Toto
Africans uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
TFF imesikitishwa na kitendo
hicho cha mashabiki wa klabu ya Simba SC, na kusema inalaani kitendo
hicho ambacho sio cha kiuana michezo, huku ikiwataka wanachama,
washabiki kuheshimu viongozi wa klabu zao waliopo madarakani na kama
kuna masuala ya kujadili wakayajadili katika vilabu vyao.
Mashabiki wa klabu ya Simba
walifanya vurugu kwa kurusha mawe, wakilenga kuwadhuru viongozi wa klabu
hiyo pamoja na wachezaji, magari waliyokuwa nayo baada ya timu yao
kupoteza mchezo dhidi ya Toto Africans kwa bao 1- 0.
Jeshi la Polisi baada ya
kuwasishi mashabiki kuondoka eneo la uwanja punde tu mchezo
ulipomalizika, mashabiki hao walikaidi na kuendelea kurusha mawe hali
iliyopelekea jeshi kutumia mabomu ya machozi kuwatanya katika eneo hilo.
Kufutia kitendo hicho, Jeshi la
Polisi lilihakikisha bus la timu ya Simba SC na viongozi wake wanaondoka
salama uwanjani baada ya kuwatawanya mashabiki hao, kwa kupitia mlango
wa karakana ya wachina waliojenga uwanja huo.
Aidha TFF imeviomba vyombo vya
Usalama na Ulinzi kuwachukulia hatua kali mashabiki waliohusika na
kitendo hicho, kwani kufanya vurugu ni kosa la jinai na wanapaswa
kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
0 maoni:
Chapisha Maoni