Mshambuliaji Shiza
Ramadhan Kichuya wa timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro amechaguliwa kuwa
mchezaji bora wa mwezi Machi kwa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa
2015/2016.
Kichuya
alionyesha kiwango cha juu katika mwezi huo uliokuwa na raundi nne,
hivyo kuisaidia timu yake kushinda mechi mbili kati ya tatu ilizocheza.
Katika
mechi hizo ambazo zote Kichuya alicheza, alifanikiwa kufunga mabao
mawili kati ya matano yaliyofungwa na timu yake. Alifunga dhidi ya
Coastal Union kwa ushindi wa mabao 3-0, na JKT Ruvu Stars ambapo Mtibwa
Sugar ilishinda mabao 2-1.
Uwezo
aliouonyesha kwa mwezi huo ulisababisha Kocha wa Taifa Stars, Charles
Mkwasa amwite kwa mara ya kwanza kwenye kikosi chake kwa ajili ya mechi
dhidi ya Chad iliyofanyika Machi 23, 2016 jijini N’Djamena.
Washindani
wa karibu wa Kichuya walikuwa washambuliaji Mbaraka Yusuf wa Kagera
Sugar, na Abdulrahman Mussa wa JKT Ruvu Stars ambao pia waling’ara kwa
upande wa timu zao kwa mwezi huo.
Kichuya
ambaye huu ni msimu wake wa pili kwenye Ligi Kuu, kwa kunyakua tuzo ya
mchezaji bora kwa Machi atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni
moja) na wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
Wachezaji
bora wa miezi mitatu iliyopita ni kiungo Thaban Kamusoko wa Yanga
(Desemba 2015), beki Shomari Kapombe wa Yanga (Januari 2016) na
mshambuliaji Mohamed Mkopi wa Tanzania Prisons (Februari 2016).
0 maoni:
Chapisha Maoni