Jumatatu, 4 Aprili 2016

TAKUKURU IRINGA YATAJA IDARA ZINAZOONGOZA KWA RUSHWA





Mkuu  wa TAKUKURU mkoa  wa Iringa Bi Eunice Mmari   akizungumza na  wanahabari  ofisini  kwake  leo
Mkuu  wa TAKUKURU mkoa  wa Iringa Bi Eunice Mmari kushoto  akizungumza na  wanahabari  ofisini  kwake  leo



Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa [TAKUKURU]  mkoani Iringa imewafikisha mahakamani watuhumiwa 4 kutokana na makosa mbalimbali yanayohusu  rushwa  katika kesi tatu zilizofikishwa mahakanai kwa kipindi cha Januari hadi machi mwaka huu 2016.
Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Takukuru mkoa wa Iringa leo hii kwa kipindi cha robo mwaka kuanzia juni hadi machi mwa huu kwa wandishi wa habari mkuu wa takukuru mkoa wa Iringa Eunice Mmari alisema katika kipindi cha muhula wa miezi mitatu takukuru ilipokea malalamiko 28 ya rushwa na 14 kati ya hayo yamefunguliwa majalada ya uchunguzi,malalamiko 9 yakifanyiwa uchunguzi wa awali na malalamiko 5 yameshindwa kuthibitishwa makosa ya rushwa.
Mmari alisema Idara zinazoongoza kulalamikiwa kwa Rushwa katika mkoa wa Iringa  katika ofisi za Takukuru nipamoja na  Idara ya Afya na serikali za mitaa pia yapo malalamiko kutoka Idara za ujenzi,kilimo pamoja na polisi kwa upande wa usalama barabarani.
Alisema watuhumiwa 4 waliofikishwa mahakani nipamoja na Lucas Daniel Mwandi ambae ni mfamasi katika Hospital ya mkoa wa Iringa aliyeshtakiwa kwa makosa ya wizi wa mali ya umma akiwa mtumishi wa umma kinyume na kifungu cha 270 sheria ya kanuni ya adhabu iliyorekebishwa mwaka 2002 katika kesi Na.53/2016.
Mwigine alifikishwa mahakani kutokana na Rushwa ni Selemani Hamza Fulano Mfamasi wilaya ya Mufindi akishtakiwa kwa makosa ya vifungu vya 22,28 na 31 katika keasi Na. 3920016.Pamoja nao wengine wengine ni Deogratias Vangilias aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Mwaya Ilula na Robert Peter Kisaka aliyekuwa Mtendaji wa kijiji cha Mwaya Ilula walioshtakiwa kwa makosa ya vifungu vya 28,31,29 NA 30 KATIKA KESI Na.23/2016,Watuhumiowa hawa wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na.11/2007.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa katika mkoa wetu wa Iringa imeendelea na utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa kufuatia sheria namba 11 ya mwak 2007.
AlisemaUtendaji wa kazi wa Takukuru mkoa wa Iringa kwa kipindi cha robo mwa januari hadi machi2016 tumetoa elimu kwa umma  kwa  wananchi wapatao 4957 kuhusu vitendo vya kupambana na rushwa ikiwa nipamoja na wanafunzi 3693 kwa njia za semina35,mikutano ya hadhara28,uimarishaji na ufunguaji wa klabu za wapinga rushwa katika shule za msingi na sekondari46,kipindi cha radio1, na kufanya onesho katika maeneo matatu ya manispaa ya Iringa katika wiki ya sheria iliyoadhimishwa februari mwaka huu,pamopja na machapisho yenye ujumbe mbalimbali wa rushwa 881 wamegawiwa kwa wananchi  ili kufikisha elimu ya rushwa.
Alisema ofisi ya Takukuru imeweza kufanya viakao vine vya kujadili dhibiti zilizofanyika ili kuziba mianya ya rushwa katika usimamizi wa mali za kijiji cha Idasi,zabuni ya ununuzi wa pumpu ya kusukuma maji katika mji wa Mafinga,ajira za vibarua katika mamlaka ya maji mji wa Mafinga na katika taratibuy za kuchukua walimu wa kujitolea shule za msingi zilizopo Manispaa ya Iringa na mfumo wa taratibu za matumizi ya fedha za mradi wa maji kijiji cha Ifunda Iringa vijijini.
Aidha alisema wameweza kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya kudhibiti mianya ya rushwa katika taratibu,usimamizi na matumizi ya vitendanisi katika Hospitali,zahanati na vituop vya Afya vilivyopo manispaa ya Iringa umefanyika katika kutekeleza majukumu yao ya kufanya uthibiti na utafiti katika maeneo yanayohusika na vitendo vya rushwa.
Alisema Takukuru Mkoa wa Iringa imeweka mikakati ya kuwafikia wananchi wengi zaidi ili kutoa Elimu ya Rushwa,kwa kufanya hivyo itaweza kusaidia wananchi kuwa na ujasili ili wajitambua kuwa na wao wanaowajibu wa kupambana na kuzuia rushwa kwa kushirikiana na Takukuru

0 maoni:

Chapisha Maoni