Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,
Nishati Ardhi na Makaazi Ali Khalil Mirza na Makamu wa Rais wa Kampuni
ya Multiconsult ya Norway Oyvi’nd Holtedahl wakipongezana mara baada ya
kusaini Mradi wa kuimarisha huduma za umeme Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji ,
Ardhi, Nishati na Makaazi Ali Khalil Mirza, akitoa maelezo juu ya mradi
wa kuimarisha huduma za Umeme Zanzibar, kabla ya kutiliana saini
makubaliano ya miaka mitatu na nusu na Serikali ya Norway katika hafla
iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara Forodhani Mjini Zanzibar.
Mshauri mwandamizi wa Kampuni ya
Multiconsult ya Norway Andrew Yager akitoa shukurani kwa Serikali ya
Zanzibar kwa kuichagua kampuni yao katika kazi za kuimarisha huduma ya
umeme katika hafla ya kutilina saini makubaliano ya mradi huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,
Nishati Ardhi na Makaazi Ali Khalil Mirza (wa kwanza kulia waliokaa)
na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Multiconsult ya Norway Oyvi’nd Holtedahl
wakitia saini makubaliano ya kuimarisha huduma za umeme Zanzibar katika
hafla iliyofanyika leo Makao Makuu ya Wizara, Forodhani Mjini Zanzibar.
……………………………………………………………………………………
Na Miza Othman-Melezo Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar,
imetiliana saini na Serikali ya Sweden makubaliano ya kuimarisha huduma
za nishati ya umeme hapa nchini.
Katika hafla ya utiaji saini wa
mradi huo, Zanzibar iliwakikishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,
Ardhi, Nishati na Makaazi Ali Khalil Mirza, wakati Makamu wa Rais
Mtendaji wa Kampuni ya Multi Consult kutoka Norway Oyvind Holtedahl,
alisaini kwa niaba ya Serikali ya Sweden.
Katika hafla hiyo iliyofanyika
Makao makuu ya Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Makaazi Katibu Mkuu
Mirza, alisema kampuni ya Multi Cionsult ilishinda zabuni hiyo kati ya
kampuni 12 zilizoomba kutekeleza mradi huo.
Alieleza kuwa mradi huo utakaochukua miaka mitatu na nusu hadi kukamilika kwake, utagharimu shilingi bilioni 12.7 za Kitanzania.
Amefahamisha kuwa, miongoni mwa
matumizi ya fedha hizo, ni kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa wizara hiyo
ili kuwajengea uwezo wa kufanya tafiti ili wafanye kazi zao kwa ufanisi.
Mirza alieleza kuwa, lengo la
Kampuni hiyo ni kusaidia katika kulijengea uwezo Shirika la Umeme
Zanzibar (ZECO) pamoja na Idara zake kuhusu sera ya nishati ambayo ni
muhimu kwa maenedeleo ya taifa.
Naye Mshauri Mwandamizi wa
Kampuni ya Multi Consult ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kwa kuwaamini kufanya kazi hiyo na ameahidi kuwa wataitekeleza kwa
ufanisi mkubwa.






0 maoni:
Chapisha Maoni