Mkuu wa mkoa wa Mwanza John
Mongella, ameagiza kurudiwa upya kwa zoezi la uhakiki la kuabaini
watumishi hewa katika mkoa wa Mwanza, ikiwa ni mpango wa kubaini wale
wote wanao lipwa mishahara bila kufanya kazi, zoezi hilo litafatia zoezi
lililo fanyika awali ambapo mkoa huo ulibainika kuwa na watumishi hewa
wapatao 334.
Mongella amesema pamoja na
kumalizika kwa zoezi la awamu ya kwanza la kuhakikiwa kwa watumishi hewa
na kubainika watumishi wapatao 334 tumeamua kufanya upya zoezi hilo ili
kuwa na idadi kamili ya watumishi wanaolipwa fedha za serikali bila
kuzifanyia kazi, Mongella, amesema tayari taratibu zinachukuliwa ikiwa
ni pamoja kuunda jopo la kuhakiki kutoka ngazi ya mkoa kwenda kwenye
halmashauri zote za mkoa wa huo kwa ajili yakufanya uhakiki upya wakiwa
na Payroll.
“Nimesha muagiza Katibu Tawala
wa Mkoa, kuwa, Wakurugenzi wote kufika kesho saa 6.00 kamili mchana
yaani tarehe 05.04.2016 (Pay roll) zote ziwe zimewasilishwa mezani
kwake, ili wataalam kutoka ngazi ya mkoa waweze kwenda nazo wilayani kwa
ajili yakufanya uhakiki upya” amesema Mongella na kuongeza ”Tunataka
kwenda kufanya uhakiki wa mtu kwa mtu (physical), popote pale walipo
warudi wahakikiwe labda kama yupo masomoni nje ya nchi.
Ameagiza wale wote walioko
masomoni, likizo au safari warudi mara moja kwenye vituo vyao vya kazi
kwa ajili ya zoezi la uhakiki, huku akiwataka wote watakao kwenda kwa
ajili ya kuhakikiwa waende wakiwa na picha tatu za passport size, ambapo
taratibu zakuweka kumbukumbu sahihi zitafanyika “Tunataka zoezi hili
lichukue muda wa siku saba tu na baada ya hapo tutatoa ripoti kamili,
tusishangae kuona idadi hiyo ikiongezeka au kupungua kwani katika
uhakiki huu naamini tutapata majibu sahihi alisema Mongella.
Aidha amesema hata kuwa na mzaha
na yeyote atakayebainika kulea matatizo ya watumishi hewa katika mkoa
huo, hivyo lazima kila mmoja awajibike kwa nafasi yake aliyo ajiriwa
nayo. Katika hatua nyingine Mongella, amevitaka vyombo vya habari katika
mkoa huo kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu
yake ya ulinzi na usalama, kusimamia maendeleo na kujua ustawi wa watu
wa Mwanza “Mwandishi wa habari hatofautiani na kachero wa Polisi, sasa
tusaidiane kuongoza huu mkoa kwakupeana taarifa, maana mkoa huu ni
mkubwa, sio rahisi kwa Mkuu wa mkoa kujua yote yanayoendelea hadi ngazi
ya kijiji lakini kwakuwa ninyi wenzangu mnao wigo huo basi tusaidiane
ili watu katika mkoa huu waweze kufanya kazi zao kwa amani na salama.
Amesema Mkuu huyo wa Mkoa wa
Mwanza. Imetolewa Atley J. Kuni AFISA HABARI NA UHUSIANO OFISI YA MKUU
WA MKOA WA MWANZA 04.April,2016






0 maoni:
Chapisha Maoni