Jumamosi, 2 Aprili 2016

SIKU YA WAJINGA DC KASESELA AWAKAMATA WANAHABARI KWA UPOTOSHAJI


 
                                    Dc  Richard  Kasesela 
.............................................................................................
         
WAKATI leo  kuanzia majira ya saa  alfajiri  hadi saa 4 ;00 asubuhi  ilikuwa ni  siku ya  wajinga  duniani ,mkuu wa  wilaya ya Iringa Bw  Richard Kasesela amewakamata wanahabari  wawili  wa  kituo  kimoja cha Radio Fm  mkoani Iringa  kwa madai ya  kuchukizwa na matumizi mabaya ya jina lake katika  kudanganya umma.


" Ahsante   sana  nimewakamata   waandishi hao  wawili kwa kosa moja kubwa ...mwandishi mmoja aliingia studio na  kujitangaza  kuwa  yeye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela na  kuanza kutoa ahadi za  kupeleka msaada wa mahindi Kipera na ahadi  nyingine  nyingi na hata  kunidhalilisha hata  mimi hii ni  sikukuu ya  wajinga ya kutaniana  zaidi na ni kosa  kutumia chombo  cha habari  kutania na ukitumia  chombo  cha  habari kutania basi ukimaliza tu kutania bila hata kupumzika  unapaswa  unapaswa  kueleza  wasikilizaji  kuwa hakuna ukweli wa jambo  hilo na ilikuwa ni  siku ya  wajinga.....wao  wametangaza kiutania  kudanganya  watu  hata  mimi nimewakamata kiutani hivyo hivyo"

Akizungumza na mtandao   huu wa KALI YA HABARI ofisini  kwake  leo  kuhusiana na hatua yake ya  kuwakamata  wanahabari  hao  wawili  alisema  kuwa hazuii chombo  cha  habari ama  mwanahabari au  mtu  yeyote  kusherekea  siku ya  wajinga japo  alisema alichochukizwa na hatua ya  chombo  hicho cha Radio Fm (jina  tunalo)  kumchukua mtangazaji mwenzao  kujifanya  ni mkuu  wa  wilaya ya kuanza kupotosha  wasikilizaji kwa  kutumia  jina na sauti  yake na mbaya  zaidi  walikuwa wakidanganya mambo ambayo ni ya kweli .

' Siku  ya  wajinga  ipo  miaka  yote ila kujiita  wewe ni fulani ama  kiongozi na  kutumia jina hilo  kudanganya  watu huo ni sawa na utapeli na upotoshaji .......kwani  hata  baadhi ya vitu  vya  kudanganya ni  vile  ambavyo haviwezi  kuhatarisha amani ama  kuchafua mwingine kwa  kisingizio  cha siku ya  wajinga....mfano  ukatangaza  kuwa polisi  wameua  watu 10 wakati ni utani unafikiri  nini ambacho kwa  utani  wako  huo unaweza kuligharimu jeshi la  polisi ....wananchi  wanaweza  kuandamana kwenda kuvamia polisi kwa  utani  wako"

Bw  Kasesela  alisema kutokana na upotoshaji  huo kwa jamii amewaita  polisi ili  kuandika maelezo yao  kwa  upotoshaji  huo  dhidi  yake na tayari  amewaachia baada ya kutoa maelezo hayo na  kuwa mbaya  zaidi  kituo  hicho  kilitangaza siku moja kabla kuwa asubuhi ya leo  watakua na mkuu wa wilaya na kimsingi siku ya  wajinga na April mosi  kila mwaka  na sio Machi 31.

 Alisema  kuwa  sikukuu ya wajinga ni masaa 4 tu na  sio zaidi ya hapo na kuwa kutokana na  kutangaza  uongo  huo amepokea simu kutoka kwa  waathirika wa Mafuriko ambao walikuwa  wakilalamika hatua ya  serikali  kuwaacha walengwa wa chakula cha msaada na  kupeleka sehemu ambayo haina shida ya chakula  cha msaada  hivyo  kuvitaka  vyombo vya habari kujenga  heshima yake kwa  kuendesha  vyombo hivyo  kitaaluma  zaidi badala ya  kuvitumia kwa upotoshaji .

Hata   hivyo waandishi haoa  wawili  tayari   wameachiwa  huru  baada ya  kuhojiwa na jeshi la polisi  sababu ya  kufanya   hivyo.

0 maoni:

Chapisha Maoni