Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo na
mtafiti wa mbegu kutoka mmoja ya maafisa wa juu wa wakala mkuu wa aghala
la mbegu za ASA(Agricultural Seed Agency) Mkoani Morogoro.
Mh.Mwigulu Nchemba akikagua mbegu zilizopo kwenye ghala la ASA mkoani morogoro.
Mwigulu
Nchemba akizungumza na watumishi wa ASA(Agricultural Seeds Agency)
wakati wa ziara hiyo,Kubwa alilosisitiza ni uzalendo na kufanya kazi kwa
kujituma.
Mh.Mwigulu
Nchemba akipewa maelekezo kuhusu malisho ya ng'ombe yanayopatikana
kwenye kituo cha utafiti wa mifugo -Morogoro(LITA).
Mh:Waziri akiangalia baadhi ya ndama wa Ng"ombe waliopo kwenye shamba la Utafiti kwenye kituo cha LITA-Morogoro.
Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na Makamu
Mkuu wa chuo za SUA(Sokoine University of Agriculture) alipofika
kwaajili ya kukutana na wataalam,na uongozi wa SUA kwaajili ya kupokea
maoni yao kuelekea kilimo,ufugaji na uvuvi wa kisasa. "Transformation of
Agriculture".
Katika kikao hicho,Wataalam kutoka SUA
walisisitiza kuwa ili Tanzania iweze kuondokana na kilimo holela,ni
wakati muafaka sasa kama nchi kuamua kuwekeza kwenye kilimo cha
umwagiliaji na kuondoakana na kilimo cha mvua,pia kuachana na jembe la
mkono na wakati huo huo kuimarisha vituo vya utafiti na kuzalisha mbegu
kikanda.
Akiwa
njiani kuelekea Ifakara,Mwigulu Nchemba anaamua kufanya mkutao Jimbo la
Mikumi kijiji cha Tungu kwaajiliya kusikiliza kero za wananchi dhidi ya
uongozi wa miwa wilaya,Mkoa na Taifa,mahusiano mabaya ya kibiashara
kati ya wakulima wa miwana kiwanda cha ilovo,Lakini utitiri wa vyama vya
wakulima kwa eneo lakilombero.
Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mbunge wa Mikumi Mh.Joseph Haule(Prof.Jay) wakati wa mkutano huo
Baada
ya kusikiliza kero kutoka kwa wananchi na kusoma baadhi ya ripoti za
serikali ya wilaya na mkoa na zile za Tume mbalimbali zilizounda kujua
kiini cha matatizo ya wakulima wa miwa-Kilombero,Mwigulu Nchemba akiwa
ndiye waziri mwenye dhamana na kilimoa akaamua kufuta uongozi wote kwa
wakulima wa miwa kuanzia ngazi ya wilaya ya Mikumi hadi Taifa kwa kosa
la ubadhilifu na matumizi mabaya ya mada






0 maoni:
Chapisha Maoni