……………………………………..
Halmashauri ya Mji wa
Kibaha Mkoa wa Pwani imeahidi kuwalipa wananchi wanaostahili kulipwa
fidia ya ardhi ambayo ilichukuliwa na Serikali kwa lengo la kutekeleza
mradi wa kitovu cha Mji wa Kibaha (CBG) unaotegemewa kujengwa katika
eneo la Machinjioni.
Akizungumza kuhusiana na
madai ya wananchi wa eneo la Machinjioni Mjini Kibaha, Afisa Habari wa
Halmashauri ya Mji huo Innocent Byarugaba amesema Halmashauri hiyo ipo
katika maandalizi ya kuitisha kikao na wananchi wa eneo la Machinjioni
ili kufanya tathmini ya wanaostahili kulipwa na kuanza utaratibu wa
kuwalipa.
Amefafanua kuwa zoezi la
kufanya tathmini katika eneo hilo lilishindikana kutokana na wafanya
tathmini kufanyiwa fujo hivyo kukwamisha utekelezaji wa zoezi hilo kwa
wakati.
“ Kabla eneo hili la
Machinjioni halijabadilishwa matumizi kutoka kuwa eneo la viwanda na
kubadilisha kuwa eneo la mradi wa kitovu cha Mji wa kibaha (CBG),
Halmashauri haikuwahi kutoa kibali kwa mwananchi yoyote kuendeleza eneo
hilo na wale wanaodai kuwa eneo hilo ni lao ni wavamizi na Halmashauri
inafanya ustarabu tu kuwalipa wale walioendeleza ili kuondoa malumbano
yaliyopo”Alisema Byarugaba.
Aidha Halmashauri ya
inaendelea kupima eneo la Machinjioni kwa hilo kwa ajili ya kuwalipa
fidia wananchi ili kupisha utekelezaji wa mradi huo.
Innocent Byarugabana
amewaasa wakazi wa Mji wa Kibaha kutovamia maeneo na kuyaendeleza bila
kuwa na hati ya umiliki wa eneo husika.
Halmashauri ya Mji wa
Kibaha ipo katika mikakati ya kuendeleza maeneo ambayo yapo katika
mikakati ya kufanyiwa miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kuhakikisha
Sheria no 2007 ya uendelezaji wa Miji ya mwaka 2008 inatekelezwa.






0 maoni:
Chapisha Maoni