TFF imeweka kiingilio cha shilingi
elfu mbili tu (2000) uwanja mzima, kutoa nafasi kwa wapenzi wa mpira wa
miguu nchini kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi kuja kushuhudia
mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu za vijana za Tanzania v
Misri.
Serengeti Boys inashuka dimbani
kucheza na The Pharaohs mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kujipima
nguvu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi na kujiandaa na mchezo wa kuwania
kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana wenye umri chini ya
miaka 17 dhidi ya Shelisheli Juni – Julai mwaka huu.
Mchezo huo wa kirafiki wa
kimataifa utachezeshwa na waamuzi wa kimataifa wenye beji za FIFA ambao
ni Israel Mjuni, akisaidiwa na Soud Lila, Frank Komba, mwamuzi wa akiba
Jonesia Rukyaa, huku kamisaa wa mchezo akiwa Isabella Kapera.
Upande wa kikosi cha timu ya Taifa
ya Misri kimewasili nchini jana mchana saa 7:30 mchana kwa shirika la
ndege la Ethiopia, kikiwa na msafara wa watu 33 wakiwemo wachezaji 25 na
viongozi 8.
The Pharaohs wanatarajiwa kufanya
mazoezi leo jioni saa 10 kamili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaa, baada ya kuwa wamefanya mazoezi jana jioni katika uwanja wa
Karume.
Kocha Shime ameishukuru TFF kwa
kufanikisha mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa, baadaya kuwa kambini na
kucheza michezo ya kirafiki na timu za ndani, wao kama benchi la ufundi
watautumia kama kipimo sahihi cha mchezo wa kimataifa katika maandalizi
ya mchezo wao dhidi ya Shelisheli.
Naye Yasser wa The Pharaohs,
ameshukuru kwa kupata nafasi ya kucheza na Tanzania mchezo wa kirafiki,
kwao ni mara ya kwanza kucheza mchezo wa kirafiki nje ya ukanda wa
Afrika Kaskazini, hivyo anaamini kesho kutakua na mchezo mzuri wenye
ushindani.
0 maoni:
Chapisha Maoni