(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
………………………………………………………………………………………..
Na EleuteriMangi-MAELEZO
Waziri wa NchiOfisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene
amewaagiza wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kuhakikisha wanampatia taarifa
ifikapo Aprili 3, 2016 ni lini mradi huo utaanza kutoa huduma.
Uamuzi huo wa Waziri Simbachawene
unafuatia makubaliano yaliyofikiwa wakati wa kikao na wadau hao Machi
31, 2016 kilichofanyika ofisi za DART jijini Dar es salaam ili
kuhakikisha wanatoa huduma ya usafiri wa uhakika kwa Watanzania na hasa
wakazi wa jiji hilo.
“Kama mambo yote yataenda vizuri
mradi huu utaanza mapema angalau mabasi 50 yaanze kutoa huduma mapema
iwezekanavyo” alisema Simbachawene.
Simbachawene alisema kuwa hadi
sasa mabasi mawili yamesha anza kufanya majaribio katika barabara za
mradi huo na kuwahimiza wadau hao waongeze idadi ya mabasi yanayofanya
majaribio angalau yafike 15 ili madereva wazoee barabara kabla ya mradi
kuanza kutoa huduma rasmi.
Ili kuongeza kasi ya kukamilisha
mradi huo, Simachawene amewataka wadau hao wa mradi wa mabasi yaendayo
haraka wawe na utaratibu wa kukutana kila siku kwa kuzingatia kazi
walizojipangia na kuangalia utekelezaji wake umefikia wapi na kumpatia
taarifa kila baada ya siku mbili.
Aidha, Simbachawene amewaasa wa
kazi wa jiji la Dar es salaam wawe watulivu kwa kuwa kazi kubwa ya mradi
huo imekamilika na mradi umekaribia kuanza kuleta matunda na hivyo
waitunze miundombinu hiyo ikiwemo barabara na vifaa vitakavyokuwa
vinatumika wakati wa kutoa huduma.
“Kuhujumu miundombinu ya DART ni
kulihujumu taifa letu, watu wote ni lazima wawe na uzalendo kwa mali yao
ili mradi uwe wa tija kwa manufaa ya nchi yetu” alisema Simbachawene.
Simbachawene amesema kuwa utunzaji
wa miundombinu hiyo utafanikiwa iwapo kutakuwa na ushirikiano mzuri
kati ya wananchi, wadau wa mradi wa DART na Serikali.
Katika kikao hicho na wadau wa
mradi wa DART, Waziri Simbachawene aliambatana na Naibu Waziri wake
Selemani Jaffo pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Mabasi ya Mradi wa Mabasi yaendayo
haraka yatakuwa yanafanya safari zake ya kutoa huduma ya usafiri kwa
wananchi kupitia eneo la Kimara, Ubungo, Morocco, Magomeni, Feri na
Kariaakoo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Takwimu UDART Hamdi Al-Hadj amesema kuwa kutakuwa na jumla ya mabasi 140
ambayo yanatarajiwa kutoa huduma katika mradi wa DART jijini Dar es
Salaam.
Kikao cha Waziri Simbachawene
kilihuwahusisha wadau wa mradi huo ambao ni DART, TANROAD, Msajili wa
Hazina, Kampuni ya Simon Group, SUMARTA, Wakala ya Serikali Mtandao
(eGA) na Jeshi la Polisi.






0 maoni:
Chapisha Maoni