WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ametembelea maeneo yaliyopendekezwa kujengwa mji wa Serikali na
kujiridhisha kuwa yanatosha kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu.
Katika ziara hiyo aliyoifanya leo
mchana (Jumatatu, Oktoba 3, 2016) Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na
ukubwa wa maeneo hayo ambayo pia yanatosha kujenga miundombinu
inayohitajika.
Katika ziara hiyo Waziri mkuu
ameridhishwa na maeneo yaliyotengwa na Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao
Makuu(CDA) yanayofaa kuwekeza kwa ujenzi wa miundombinu ya biashara kama
masoko na hoteli na viwanda na tumejirishisha kuwepo kwa ardhi ya
kutosha.
Wakati huo huo Waziri Mkuu
amekaribisha wawekezaji wa miradi mbalimbaliya maendeleo ikiwemo ya
ujenzi wa nyumba za watumishi ambao watajenga nyumba za makazi na
kuziuza kwa watumishi wa umma na wananchi.
Aidha amebainisha kuwa
muwekezaji atakayekuwa tayari awasiliane na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,
Jordan Rugimbana ambaye ndiye anayeratibu shughuli hiyo huku
akikaribisha wawekezaji wa ujenzi wa hoteli za kitalii na kawaida kwa
kuwa wanatarajia kupata wageni wengi.
“Tumekaribisha pia wawekezaji wa
ujenzi wa viwanda tumeiona ardhi inatosha na uzalishaji ni mkubwa Kanda
ya kati kwa mkoa wa Dodoma wenyewe, Manyara, Singida na mikoa ya jirani
ya Iringa na Morogoro inaweza kunufaika na fursa hizo,” amesema.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), Mhandisi
Paskasi Muragili alisema maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi huo
ambayo Waziri Mkuu alimeyatembelea ni Chigongwe lenye hekta 11,297,
Kikombo hekta 13,275 na Nyankali hekta 2,370.
0 maoni:
Chapisha Maoni