Posted by Esta Malibiche on Oct4.2016 in NEWS
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Bw.Senzo Gwanchele (wa pili
kushoto) akifafanua jambo kwa viongozi na watendaji wa wakala huo
(hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao,
Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa idara ya ushauri wa
kitaalam wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Eng. Manase LeKujan (wa
pili kulia) akizungumza na viongozi na watendaji wa wakala huo (hawapo
pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar
es salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA),Dkt.Musa Mgwatu (Katikati) akitoa maelekezo kwa
viongozi na watendaji wa wakala huo (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi
wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam.
Viongozi na Watendaji wa Wakala
wa Ufundi na Umeme (TEMESA), wakimsiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt.Musa Mgwatu (hayupo pichani) wakati wa
ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………
Na Theresia Mwami TEMESA.
Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wameshauriwa kujituma kwa bidii katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.
Ushauri huo umetolewa leo na
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt Musa Mgwatu alipokutana na watumishi hao
kutoka katika Mikoa/vituo vya TEMESA vilivyopo nchi nzima katika kikao
kazi kilichofanyika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Dkt Musa Mgwatu amesema kuwa ana
muda mchache tangu aanze kutekeleza majukumu yake na ameanza kujifunza
mambo mbalimbali kuhusu Wakala huu na kuahidi kupita katika vituo
vilivyopo mikoani ili aweze kujifunza zaidi.
“Naahidi kushirikiana nanyi
katika kuijenga TEMESA Mpya na naomba ushirikiano wenu na muwe
wafatiliaji wa mambo kwani kazi zetu zinahitaji sana ufatiliaji wa kina”
Alisema Dkt Mgwatu.
Ameongeza kuwa amepanga mikakati
ya kuiimarisha TEMESA katika maeneo ya Matengenezo ya magari kwenye
karakana za TEMESA, namna ya kuyatambua madeni ya TEMESA pamoja na
utunzaji wa taarifa zake, utendaji kazi chini ya kiwango wa baadhi ya
karakana, mawasiliano kati ya TEMESA makao makuu na mikoa au vituo vyake
na utendaji kazi na watu au kampuni zilizosajiliwa.
Amesisitiza kuwa watumishi
wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa dhana potofu iliyojengwa
juu ya TEMESA kwa wateja wake, wajiimarishe katika utendaji kazi kwa
kasi, ubora, weledi uadilifu, ufuatiliaji, na uwajibikaji.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
wa Huduma za uendeshaji TEMESA Bw. Senzo Gwanchele amesema kuwa kikao
kazi hicho kimelenga kuondoa baadhi ya matatizo yanayojitokeza katika
utendaji wa kila siku ikiwemo hoja mbali mbali za ukaguzi, ulipaji wa
kodi ya ongezeko la thamani (VAT) pamoja na uzingatiaji wa sheria ya
Ununuzi wa Umma.
Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA) hivi karibuni imepata Mtendaji Mkuu mpya ambaye amekuja na
mikakati ya kujenga na kuimarisha TEMESA kwa kupambana na changamoto
zinazoikabili Wakala kwa sasa.
0 maoni:
Chapisha Maoni