Posted by Esta Malibiche on Oct3.2016 in NEWS
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa
Mohamed Chande Othman akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo
pichani) kabla ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na ile ya Afrika
Mashariki na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo ofisini
kwake leo jijini Dar salaam.
Mpicha Chapa Mkuu wa Serikali,
Kassian Chibogoyo akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa
Mohamed Chande Othman kabla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa na Ile ya
Afdrika Mashariki leo katika Ofisi ya Jaji Mkuu jijini Dar es salaam
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa
Mohamed Chande Othman akikabidhiwa Bendera ya Taifa na Mpiga Chapa Mkuu
wa Serikali, Kassian Chibogoyo leo ofisini kwake jijini Dar salaam
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa
Mohamed Chande Othman akikabidhiwa Bendera ya Afrika Mashariki na Mpiga
Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo leo ofisini kwake jijini Dar
salaam
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa
Mohamed Chande Othman akifurahia Zawadi ya Tai ya Bendera ya Taifa
aliyopewa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Kassian Chibogoyo leo
ofisini kwake jijini Dar salaam
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa
Mohamed Chande Othman akimwonyesha Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kitabu
cha Sheria kuhusu matumizi ya Vielelezo vya Taifa kabla ya kukabidhiwa
Bendera ya Taifa na ile ya Afrika Mashariki.
………………………………………….
Na Mary Gwera, MAHAKAMA
JAJI Mkuu wa Tanzania, Mhe.
Mohamed Chande Othman amezitaka Wizara, Halmashauri na Taasisi nyingine
za Serikali kutumia vielelezo vya Taifa kama bendera na nembo ya taifa
katika ofisi zao ili kuenzi tunu na vielelezo vya Taifa.
Aliyasema hayo ofisini kwake
Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam alipokuwa akipokea rasmi bendera
ya Taifa na Afrika Mashariki kutoka kwa Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali,
Bw. Cassian Chibogoyo.
Alisema kuwa vielelezo hivi vya taifa vinalindwa kisheria kwa hiyo inabidi vipate heshima yake kwa kuwa vinawakilisha taifa.
“Sheria pia inavitambua vielelezo
hivi hivyo ni muhimu vikapewa heshima yake, kwani hata mtu akichezea
vitu hivi anaweza kufungwa kwa mujibu ya sheria,” alisisitiza Jaji Mkuu.
Aliongeza pia Mahakama ya
Tanzania pia iko katika mchakato wa kupata bendera yake kama ilivyo kwa
Taasisi nyingine kama Bunge, pamoja na nembo yake ili ziweze kutumika
katika Mahakam azote nchini.
Awali; akiongea na Jaji Mkuu
pamoja na waandishi wa habari kabla ya makabidhiano hayo, Mpiga Chapa
Mkuu wa Serikali, Bw. Cassian Chibogoyo pia alizitaka Taasisi za
Serikali kutopuuzia umuhimu wa matumizi wa vielelezo vya Taifa.
Alisema kuwa baadhi ya Ofisi
nyeti za Serikali hazina bendera na vielelezo vingine muhimu ambavyo
vinaiwakilisha Taifa na kusisitiza matumizi yake ili kuenzi tunu za
Taifa.
“Ofisi nyingi za Serikali
zinatumia bendera zilizochakaa na nyingine hazina kabisa, vitu hivi ni
muhimu kwa taifa hivyo ni vyema kuvienzi na kuvithamini pamoja na
kuvitunza,” alisema Bw. Chibogoyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni