Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dk. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Erasto Aron
Mfugale kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba kuziba nafasi iliyoachwa
wazi na Bw. Stephen Makonda ambae uteuzi wake ulitenguliwa na Mhe.
Rais tarehe 27.9. 2016.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe kwa Vyombo vya Habari imeeleza kuwa kabla
ya Uteuzi huo wa Bw. Erasto Mfugale alikuwa Mkuu wa Idara ya Ustawi wa
Jamii katika Halmashauri ya mji wa Masasi.
Uteuzi wa Bw. Mfugale unaanza mara moja.
0 maoni:
Chapisha Maoni