Jumatano, 17 Agosti 2016

Waziri wa Viwanda Mh Charles Mwijage azindua Upanuzi wa kiwanda cha saruji TANGA

TAN1
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, akizindua rasmi upanuzi wa kiwanda cha saruji Tanga (Tanga Cement Company Ltd.) upanuzi huo umehusisha kuongeza Tanuri no. 2 (Kiln no. 2) ambapo uzalishaji utaongeza hadi kufikia tani mil. 1.25 kwa mwaka, kiwanda kimewekeza dola za kimarekani mil. 152 katika kufanikisha upanuzi huo.
TAN2
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, akihutubia mara baada ya upanuzi wa kiwanda cha saruji Tanga (Tanga Cement Company Ltd.), shughuli hii ilihudhuriwa na Viongozi, Wabunge wa Mkoa wa Tanga, Wafanyakazi wa Kiwanda na Uongozi wa Kiwanda.
TAN3
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha saruji cha Tanga Bw. Lawrence Masha.
TAN4
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa upanuzi wa kiwanda.
TAN6
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi huo
TAN7
Mkurugenzi mtendaji wa Kiwanda cha saruji cha Tanga Ndugu. Reinhardt Swart akihutubia wakati wa mkutano huo.
TAN8
Mku wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Ndugu, Martin Shigella Akihutubia katika uzinduzi huo.

0 maoni:

Chapisha Maoni