Postedy by Esta Malibiche on August 26.2016 in News
Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic Party
(UDP) John Momose Cheyo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo
pichani) kuhusu hali ya kisiasa nchini katika mkutano uliofanyika katika
ukumbi wa Idara ya Habari – Maelezo leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – Maelezo Tiganya Vicent.
Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic Party
(UDP) John Momose Cheyo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo
pichani) kuhusu hali ya kisiasa nchini katika mkutano uliofanyika katika
ukumbi wa Idara ya Habari – Maelezo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – Maelezo Tiganya
Vicent na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama hicho Goodlucky Ole Medeye.
………………………………………………………………………………
Na: Lilian Lundo -MAELEZO
Dar Es Salaam
Mwenyekiti wa Chama cha UDP John
Cheyo amewataka Watanzania kupaza sauti na kukataa maandamano ya
Septemba Mosi mwaka huu ambayo yameandaliwa na Chama cha Demokrasia
(CHADEMA).
Cheyo ameyasema hayo leo jijini
Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu msimamo
wake juu ya maandamano hayo.
“Watanzania wenzangu jambo la
kuwaacha watoto wetu kwenda kupambana na Polisi si jambo zuri, wote
tupaze sauti zetu na kusema hapana kwa maandamano ya Septemba Mosi,”
alisisitiza Cheyo.
Alisema kuwa, ziko njia mbalimbali
ambazo Chadema wanaweza kuzitumia kutatua migogoro, kama vile meza ya
mazungumzo na kuachana na maandamano ambayo yanachochea vurugu na hata
kutishia amani ya nchi.
Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi
linapotoa katazo la maandamano ni lazima utii uwepo, kwani Polisi wapo
kwa mujibu wa Sheria na Katiba. Ikiwa Chama hicho hakikuridhika na
katazo hilo basi wanatakiwa kuonana na Waziri anayehusika na Jeshi la
Polisi.
Akifafanua zaidi alisema kuwa Rais
Magufuli amekuwa akichukua hatua za makusudi za kutatua matatizo
mbalimbali kama vile kupambana na ufisadi, ambapo viongozi wengi wa
Serikali wamesimamishwa kazi au kufukuzwa kutokana na kujihusisha na
masuala ya rushwa.
Mwenyekiti huyo wa UDP amewataka
watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Magufuli ili aweze kutimiza ndoto
zake na yale ambayo ameyaahidi kwa ajili ya nchi ya Tanzania.
Aidha Cheyo aliwasifu viongozi wa
Dini ambao walikaa na Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)
na kukubali kurudi bungeni bila pingamizi lolote. Amewataka viongozi
hao wa dini kuendelea kuzungumzia suala la amani kwa Watanzania na
Viongozi wa kiasa ili kudumisha amani ya nchi.
0 maoni:
Chapisha Maoni