Mkurugenzi
wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline
Mengi (wa pili kushoto) akiwa ameongoza na Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Raymond Mapunda (kushoto), Diwani wa Kata ya Mwananyamala,
Songoro Mnyonge (wa tatu kushoto) pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Msingi Kinondoni, Emmanuel Ntenga mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline
Mengi akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kinondoni ambapo
aliwahimiza kusoma kwa bidii vitabu hivyo ili kupanua ufahamu wao zaidi
na hata kimasomo pia vitasaidia kuinua viwango vyao vya ufaulu.
Mkurugenzi
wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline
Mengi na uongozi wa shule hiyo kwa pamoja wakiimba na wanafunzi wa shule
ya Msingi Kinondoni.
Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline
Mengi akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi wa
maktaba ya vitabu aliyoipa jina la Dr. Ntuyabaliwe Foundation katika
hatua za kumuenzi marehemu baba yake ambaye aliyemjengea misingi mizuri
ya usomaji wa vitabu wakati wa makuzi yake
Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline
Mengi akionyesha wageni waalikwa picha mbalimbali za awali kabla ya
kukarabati maktaba hiyo.
Afisa
Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda akikata utepe kuashiria
uzinduzi rasmi wa maktaba ya Shule ya Msingi Kinondoni jijini Dar es
Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline
Mengi (katikati) pamoja na Diwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro
Mnyonge.
Afisa
Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda na Mkurugenzi wa Dr.
Ntuyabaliwe Foundation, Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi kwa
pamoja wakizundua nembo ya taasisi hiyo.
Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi
wakipeana mikono na Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond
Mapunda.
Miss
Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akimwonyesha baadhi ya vitabu Afisa
Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda vinavyopatikana katika
maktaba hiyo.
Miss
Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akifurahi katika picha ya pamoja na
baadhi ya walimu wa shule hiyo wakati akiondoka shuleni hapo.
Na Mwandishi wetu
Kwa kutambua
umuhimu wa elimu kwa kizazi cha sasa na baadae, Jacqueline Mengi kupitia
Taasisi yake ya Dk. Ntuyabaliwe ameamua kuunganisha nguvu kwa serikali
ya awamu ya tano iliyo chini ya Rais Magufuli kwa kusaidia kuboresha
upatikanaji wa elimu bora kwa kufanya marekebisho ya maktaba katika
shule ya msingi Kinondoni.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo ambao uliambatana na uzinduzi wa Taasisi
ya Dk. Ntuyabaliwe, Jacqueline amesaidia kufanya ukukarabati wa maktaba
katika shule hiyo na kuweka vitabu ikiwa ni sehemu ya kumkumbuka baba
yake Dk. Ntuyabaliwe kutokana na kupenda kwake kusoma vitabu.
Alisema baba
yake alikuwa akiamini zaidi katika vitabu hivyo alipenda hata watoto
wake wasome vitabu na anachokifanya yeye kwa sasa ni kuendeleza juhudi
ambazo alikuwa akiifanya baba yake ya kuona watu wakisoma vitabu na
matarajio yake ni kuona vitabu hivyo vikiwasaidia wanafunzi wa shule
hiyo kuwaongezea uwezo wa kufaulu katika masomo yao ya darasani.
"Ndoto yangu ya
muda mrefu leo imetimia, kila mtu ambaye alikuwa akimfahamu baba yangu
Dk. Ntuyabaliwe alikuwa akifahamu kuwa alikuwa anapenda vitabu na hata
sisi alituzoesha kusoma vitabu na hata kuanzishwa kwa taasisi hii ni
sehemu ya kumkumbuka yeye,
"Naamini kuwa
usomaji wa vitabu unaweza kumsaidia mtu kufika mbali hata kama sio
katika elimu unaweza kumsaidia kwa jambo lingine hata katika maisha ...
ndoto yangu ni kuona watanzania wote wanapenda kusoma kama baba yangu
alivyokuwa anapenda kusoma vitabu," alisema Jacqueline.
Nae mgeni rasmi
katika shughuli hiyo, Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond
Mapunda alisema sio jambo rahisi serikali kuweza kumaliza changamoto
zote zilizopo na kupitia watu wenye moyo kama wa Jacqueline ambao
wanaunga mkono juhudi za serikali kunaweza saidia upatikanaji wa elimu
bora.
Alisema kupitia
maktaba hiyo anaamini ipo siku kutatokea mtu ambaye atakuwa na msaada
kwa Tanzania ambaye wakati akisoma alikuwa akitumia maktaba ambayo
imefanyiwa ukarabati na Jacqueline Mengi.
"Nimeona hali
ambayo ilikuwa awali katika eneo hili na niseme tu Jacqueline atakuwa na
yeye aliguswa na hali hiyo na nitumie fursa hii kumshukuru sana kwa
msaada ambao ameutoa, shule inatakiwa kutoa elimu bora lakini ili
kufikia malengo hayo kunahitajika kuwe na nyenzo za kutosha ambazo
zitasaidia malengo ya kielimu kufikiwa," alisema Mapunda.
Kwa upande wa
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kinondoni, Emmanuel Ntenga alimshukuru
Jacqueline Mengi kwa msadaa wa kukarabati maktaba ya vitabu ili
wanafunzi kujisomea, maktaba ambayo awali hawakuwahi kuwa nayo.
"Tunakushukuru
sana kwa maktaba hii sasa wanafunzi wataweza kujisomea, tunafahamu
juhudi za Dk. Mengi katika kusaidia elimu kwa kutoa madawati sasa na
wewe umemuunga mkono tunawashukuru kwa hilo," alisema Ntenga.
0 maoni:
Chapisha Maoni