Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia
Mjema akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala wakati
alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya
hiyo ambapo uchunguzi wa wanafunzi wengine hewa bado unaendelea.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia
Mjema akisisitiza jambo wakati alipozungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake Ilala wakati alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa
599 katika shule 6 za wilaya hiyo, Kulia ni Mkurugenzi wa Wilaya hiyo
Bw. Edward Mpogolo.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia
Mjema akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake Ilala wakati alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa
599 katika shule 6 za wilaya hiyo.
…………………………………………………………………………………………………..
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia
Mjema ametangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za
wilaya ya Ilala ambazo hakuzitaja, Mjema amesema baada uchunguzi huo
kumegundulika wanafunzi idadi hiyo ya ambapo wahusika wote
watachukuliwa hatua za kinidhamu lakini pia sheria itachukua mkondo wake
kwani hayo ni makosa kama yalivyo makosa mengine
Wilaya ya Ilala ina shule za
sekondari za serikali 46 na za sekondari 49 ukiacha shule za taasisi
binafsi ,zoezi la ukaguzi bado linaendelea katika shule zote za msingi
wilayani humompaka Septemba 1 mwaka huu ndiyo litamalizika.
Akizungumzia suala la Madawati
mkuu wa wilaya huyo amewapongeza wadau wote waliochangia madawati mpaka
kuhakikisha uhaba wa madawati katika wilaya ya Ilala unakwisha huku
kukiwa ziada ya madawati 2821
Ameongeza kuwa kazi kubwa inayofuatia kwa sasa ni kuongeza vyumba vya madarasa ambapo kazi hiyo inaendelea vizuri .
Mh. Sophia mjema pia amemshukuru
Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuanzisha mkakati wa wadau kuchangia
madawati jambo ambalo limesaidia tatizo hilo kushughulikiwa kikamilifu
na wadau mbalimbali, lakini pia akampongeza Mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam Mh. Paul Makonda kwa usimiamizi thabiti wa utekelezaji wa mkakati
huo jambo ambalo limesaidia wilaya ya Ilala kumaliza kabisa tatizo la
uhaba wa madawati katika shule za zake za msingi
0 maoni:
Chapisha Maoni