Postedy by Esta Malibiche on August 25.2016 in News
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wa halmashauri na Maofisa
Elimu nchini kutowaondoa katika nyadhifa zao Waratibu wa Elimu Kata na
Wakuu wa shule za sekondari wasiokuwa na shahada, walimu wakuu wa shule
za msingi wasiokuwa na diploma badala yake wawahamasishe kwenda kusoma.
“Maofisa Elimu na Wakurugenzi
msije mkawaondoa wale walimu wakuu kwa zile sifa nilizosema bado muda
ukifika tutatangaza.Msije mkawakurupusha sasa hivi waacheni waendelee na
kazi zao tutatoa muda ili wajipange viziri,” aliema.
Agosti 20 mwaka huu Waziri Mkuu
alisema Waratibu wa Elimu katika ngazi ya Kata na Wakuu wa shule za
sekondari wanatakiwa kuwa na shahada huku walimu wakuu kwenye shule
wanatakiwa kuwa na diploma.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana
jioni (Jumatano, Agosti 24, 2016) wakati akizungumza na wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha Mandela katika jimbo
la Sumbawanga mjini.
Alisema Mratibu wa Elimu katika
ngazi ya Kata ni lazima awe na shahada ili aweze kutekeleza majukumu
yake ya kusimamia utolewaji wa elimu katika shule za sekondari na
msingi.
“Wakuu wa shule za sekondari na
waratibu wa elimu kata wasiokuwa na shahada wasiondolewe katika nafasi
zao kabla ya kupewa nafasi ya kwenda kujiendeleza kwa masomo ili waweze
kuwa na vigezo vya kuendelea kushika nyadhifa hizo,” alisema.
Alisema katika kuboresha maslahi
ya walimu Serikali imetenga zaidi ya sh. bilioni tano kwa mwezi ambazo
ni posho ya madaraka. Waratibu Elimu Kata wanapewa sh 250,000 kwa mwezi
huku Wakuu wa shule za sekondari na walimu wakuu katika shule za msingi
wanapewa sh. 200,000.
Waziri Mkuu alisema badala ya
kuwaondoa kwenye nyadhifa hizo ni vema Wakurugenzi wakawahamasisha
walimu hao kwenda kusoma ili na wao wanufaike na posho ya madaraka
iliyoanza kutolewa na Serikali hivi karibuni.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu
amewataka wazazi na walezi kwenda kuwaandisha watoto wenye umri wa miaka
mitano katika shule za awali ambapo watapata fursa ya kujengewa msingi
mzuri wa masomo kabla ya kuanza darasa la kwanza.
Pia aliagiza shule zote za msingi
nchini zisizokuwa na madarasa ya awali kuhakikisha waanzisha madarasa
hayo haraka na kuanza kutoa elimu hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni