Jumanne, 23 Agosti 2016

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI SINDE JIJINI MBEYA WAPO HATARINI KUUGUA MAGONJWA YA MLIPIKO




Wanafunzi wa Shule ya Msingi Sinde Kata ya Sinde katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, mkoani Mbeya wa kunywa maji kwenye chemchem ya maji wakati wa mapumziko jana. Wanafunzi hao wako hatarini kuugua magonjwa ya mlipuko kutokana na kunywa maji yasio safi na salama kutoka kwenye Korongo la maji lililopo karibu na shule hao kama ilivyokutwa na mpigapicha wetu. Korongo hilo maarufu kwa jina la Afrika linatumiwa pia na wakazi wa eneo hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya majumbani. Wanafunzi hao waliambia mpigapicha wa gazeti hili kuwa wapo baadhi ya wenzao ambao wameugua ugonjwa wa Kichocho pamoja na homa ya matumbo kutokana na kunywa maji hayo. Shule ya Msingi Sinde pia inakabiliwa na ukosefu maji ya bomba pamoja na ubovu wa miuudombinu ya vyoo vya wanafunzi.

0 maoni:

Chapisha Maoni