Postedy by Esya Malibiche on August 27.2016 in World News
……………………………………………………………….
CHANZO BBC
Ibada
ya wafu imefanyika nchini Italia kwa ajili ya watu 290 waliofariki
dunia katika tetemeko kubwa lililoikumba nchi hiyo siku ya Jumatano wiki
hii.
Siku ya kitaifa ya maombolezi
imeanza nchini Italia, kuwaomboleza waathiriwa wa tetemeko kubwa la
ardhi, lilokumba maeneo ya katikati mwa taifa hilo.
Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi
amehudhuria mazishi ya mazishi ya kitaifa ya waliofariki dunia katika
eneo lililopata pigo kubwa, Arquata.
Hali ya tahadhari imetangazwa katika maeneo yaliyoathirika.
Zaidi ya watu 280 wanaaminika kwamba wameaga dunia.
Takriban watu 400 kwa sasa wanatibiwa hospitalini.
Matumaini ya kupata watu wakiwa hai kwenye vifusi vya majengo yaliyobomolewa yanafifia baada ya siku tatu za uokoaji.
Raia wengi wa Italia waliaga dunia, pamoja na raia kadhaa wa kigeni.
Bendera ya taifa hilo inapeperushwa nusu mlingoti.
Zaidi ya watu 200 waliuwawa katika eneo la Amatrice pekee.
Watu 2,000 wameachwa bila makao.
Tetemeko la ardhi lilikuwa na
nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter, lilitokea mapema jumatano,
kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Italia Roma.
0 maoni:
Chapisha Maoni