Postedy by Esta Malibiche on August 19.2016
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
MAELEZO,Hassan Abbasi akijibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa
kuhusiana na mikakati yake ambayo aliitaja,kulia ni Mkurugenzi Msaidizi,
Vicent Tinganya.
……………………………………………………………………
Serikali kupitia Idara ya
Habari-MAELEZO itaanza kutekeleza mikakati mbalimbali inayolenga
kuwapatia wananchi taarifa za kila mara kuhusu utekelezaji wa ahadi
zake. Mikakati hiyo itakayosaidia kuongeza uwazi na ushirikishaji,
pamoja na mambo mengine, itahusisha hatua zifuatazo:-
Mosi, kuboresha mfumo wa mawaziri
na watendaji waandamizi Serikalini kuzungumza na wananchi ili kuainisha
utekelezaji wa vipaumbele vya bajeti, sera na mipango ya Taifa. Kuanzia
Agosti 25 mwaka huu, mawaziri wataanza kuzungumza na umma kupitia vyombo
vya habari kueleza vipaumbele vya bajeti zao na utekelezaji wake hadi
kufikia sasa.
Pili, kuanzisha utaratibu wa Idara
ya Habari-MAELEZO kueleza kwa umma kila mara, na haraka iwezekanavyo,
utekelezaji wa sekta zote katika ngazi ya kitaifa. Msemaji Mkuu wa
Serikali atakuwa akitoa taarifa hizo kuanzia hivi karibuni.
Tatu, Serikali itaimarisha
ushirikiano zaidi na wadau mbalimbali katika kutekeleza mikakati yake ya
mawasiliano kwa umma. Pamoja na wadau wengine, Serikali itahakikisha
inafanyakazi kwa karibu na vyombo vya habari ili vishiriki vyema katika
ujenzi wa Taifa.
Mwisho, wakati huu Idara
ikiendelea kufanyiakazi mikakati mingine ili kuboresha mawasiliano kwa
umma, naomba wadau wote kutoa ushirikiano kwangu binafsi, Idara
niliyopewa kuiongoza hivi karibuni na zaidi tumuunge mkono Mhe. Rais
Dkt. John Pombe Magufuli katika ajenda yake ya mageuzi kupitia HapaKaziTu.
Imetolewa na:
Hassan Abbasi,
Mkurugenzi Idara ya Habari-MAELEZ
0 maoni:
Chapisha Maoni