Postedy by Esta Malibiche on August 22.2016 in KITAIFA with No comment
Wasanii wa kijiji cha Katumba
wilayani Mpanda wakicheza ngoma ya Kasimbo wakati Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo akiwa katika
ziara ya mkoa wa Katavi Agosti 21, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary
Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Mpanda wakati Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadahara kwenye uwanja wa Kashaulili
mjini Mpanda Agosti 21, 2016. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja
Jenerali Mstaafu, Raphael Mbuga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwahutubia wananchi wa Mpanda wakati kwenye mkutano wa hadhara
uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda Agosti21, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
mkewe Mary (kulia kwake) wakiwapungia wananchi wa Mpanda wakati
walipowasili kwenye uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda kuhutubia mkutano
wa hadhara Agosti21, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewataka watendaji wa halmashauri mkoani Katavi kuwa makini na matumizi
ya fedha za maendeleo zinazopelekwa katika maeneo yao na atakayethubutu
kuzichezea zitamuunguza.
“Fedha hii tafadhali ni ya moto.
Msicheze na hii ya halmashauri tunayoileta hapa halmashauri kwa ajili ya
wananchi itawakunguza vidole. Tunaileta kwa madhumini, tunataka
wananchi wahudumiwe,“ alisema.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana
jioni (Jumapili, Agosti 21, 2016) wakati akihutubia umati mkubwa wa
wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Azimio
wilayani Mpanda.
Alisema Serikali imeanza kupeleka
fedha za miradi ya maendeleo katika halmashauri mbalimbali hivyo ni vema
kila mtendaji ahakikishe fedha hizo zinatumika kwa ajili ya ujenzi wa
miradi iliyokusudiwa na si vinginevyo.
Waziri Mkuu alisema ni lazima
wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri wahakikisha viwango vya
ubora wa miradi inayojengwa katika maeneo yao kuwa inalingana na thamani
halisi ya fedha zilizotolewa
Wakati huo huo Waziri Mkuu
amemtaka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu kwenda wilayani Mpanda na kuangalia namna ya kuipanua
hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambayo inahudumia mkoa wote wa Katavi.
Alisema hospitali hiyo ilijengwa
mwaka 1957 kama zahanati ambayo kwa sasa yanatumika katika kuwahudumia
wananchi wate wa mkoa huo imezidiwa hivyo alimuagiza mkuu wa mkoa huo
Meja Jenerali (Mstaafu) Raphael Muhuga kuharakisha ujenzi wa hospitali
ya mkoa.
Aidha, Waziri Mkuu alisema kuwa
wakati mkoa ukiwa kwenye harakati za ujenzi wa hospitali ya mkoa wilaya
nazo zianze ujenzi wa hospitali za wilaya ili kuhakikisha sera ya
Serikali ya kuwa na hospitali katika kila wilaya inatekelezwa.
Alisema kwa sasa madaktari na
wauguzi wanaofanya kazi kwenye hospitali ya Manispaa ya Mpanda
wamezidiwa kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa kuliko uwezo
wao. Hivyo amewataka madaktari na wauguzi wa wilaya ya Mpanda kuendelea
kufanya kazi kwa kushirikiana na wenzao wa Manispaa.
Awali hospitali hiyo ilikuwa chini
ya uongozi wa halmashauri ya Mpanda. Hospitali hiyo kwa sasa ipo chini
ya Manispaa ya Mpanda hivyo Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa mkoa huo
kuboresha huduma kwa kupeleka dawa na vifaa tiba vitakavyoweza hospitali
hiyo kuhudumia wagonjwa wa mkoa.
Mkoa umetenga sh. bilioni 1.7 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya mkoa.
0 maoni:
Chapisha Maoni