Postedy by Esta Malibiche on August 28.2016 in News
Na Sheila Simba- MAELEZO
Waziri wa Aridhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa Serikali imeanza kazi ya
kupima ardhi nchi nzima kuanzia mkoani Morogoro.
Akizungumza katika kipindi kipya
cha “TUNATEKELEZA” kinachoandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO na TBC1
,alisema utekelezaji wa zoezi hilo umeanzia mkoani humo ili kupima
maeneo ya wakulima na wafugaji na kutatua migogoro ya ardhi Mkoani humo.
“Serikali tumedhamiria kumaliza
migogoro ya ardhi, kutimiza ndoto ya Rais Magufuli ya kuondokana na
migogoro ya ardhi isiyo na tija inayosababisha watu kupoteza
maisha’’Alisema Lukuvi
Ameongeza kuwa katika upimaji huo
wa ardhi serikali inashirikiana na kampuni binafsi zilizosajiliwa ili
kumuwezesha mwananchi anayemiliki shamba,kiwanda ,mkulima na mfugaji
mwenye eneo kupimiwa na kuongezewa thamani.
“Nakuhakikishia katika kipindi
cha miaka 10 kila kipande cha ardhi Tanzania kitakuwa kimepangwa na
kupimwa utaratibu mzuri utakao mwezesha kila mtumiaji wa ardhi kutumia
eneo lake”alifafanua Lukuvi.
Pia ameeleza suala la kuthibiti
bei ya kupima ardhi kwa kushirikiana na wapimaji binafsi katika kumfanya
kila mtanzania alipe bei halali ya kupima ardhi.
Aidha amesme kuwa Serikali itaweka
ukomo wa kumiliki ardhi ili kuondoa tabia za watu kumiliki eneo kubwa
la ardhi bila ya kuliemdeleza kwa muda mrefu.
“serikali itaweka muda wa mtu kumiliki ardhi, haiwezekani mtu mmoja amiliki eneo hata bila kulitumia, tabia hii itafika mwisho.”
Akizungumzia suala la wageni
kumiliki ardhi alisema kuwa ni marufuku kwa wageni na wawekezaji kununua
ardhi vijijini bila kupitia wizara inayohusika.
“Ni marufuku kwa mgeni au
mwekezaji kwenda kijijini kununua ardhi bila kuja kwangu au Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC),wakifanya hivyo tutawapa ardhi wawekeze, Pia
mtu yeyote anayetaka kujenga kiwanda popote afike ofisini kwangu
nitampatia ardhi ndani ya siku saba.”alisema Lukuvi
Ameongeza kuwa Wizara imetenga
viwanja 240 kwa ajili ya Viwanda enoa la Kigamboni ili kutimiz lengo la
Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.
Mbali na hayo Waziri Lukuvi
alisema wananchi wote waliodhulumiwa viwanja Jijini Dar es Salaam kwa
makosa ya watendaji wa Serikali wameanza kupewa viwanja vingine
mbadala.
“Naagiza Halmashauri zote ziwapatie viwanja mbadala wananchi ambao walidhulimiwa viwanja vyao kwa makosa ya watendaji.”
0 maoni:
Chapisha Maoni