Jumanne, 30 Agosti 2016

WASHINDI WA DANCE BATTLE ZONE (MPAMBANO WA DANSI), KWA MKOA WA DAR ES SALAAM WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO


Postedy by Esta Malibiche on August 30.2016 in BURUDANI
2
Mkurugenzi, UDO East Africa Ashraf Rwabigimbo akimkabidhi Amani Hamisi mfano wa hundi ya shilingi milioni moja mshindi wa shindano la dansi kutoka kundi la  BITZ – House of Kinetix  lililofanyika mwezi huu jijini Dar es salaam, katikati ni Idris SD Mkurugenzi wa Fedha UDO East Africa.
3
Mkurugenzi, UDO East Africa Ashraf Rwabigimbo akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es salaam kuhusu ushindi wa Amani Hamisi aliyekaa kushoto, kulia ni  Idris SD Mkurugenzi wa Fedha UDO East Africa.
…………………………………………………………………………
Dance Battle Zone ni shindano la Mpambano wa Dansi linalo andaliwa na kuendeshwa na United Dance Organization (UDO)- East Africa.
UDO East Africa ni sehemu ya Mtandao wa shirika linalo andaa mashindano ya dance duniani, linalo fahamika kama United Dance Organization (UDO) lenye makazi yake jijini Cardif Nchini Uingereza.
Shindano hili linawahusisha vijana wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea na linafanyika kwa awamu mbili na kwa upande wa Tanzania litafanyika katika awamu mbili, ya mkoa na awamu ya pili itakuwa ni ya Kitaifa na litashirikisha jumla ya mikoa mine (4) kwa kuanzia.
Kwa mkoa shindano hili limeanzia na mkoa wa Dar es Salaam, ambapo shindano hili lilizunduliwa rasmi na Mheshimiwa Mbunge wa Mikumi, Jospeh Haule almaarufu kama Prof J. mnamo August 7, 2016 na kumalizika 28 August, na Mshindi wa Dar es Salaam ni kundi la BITZ – House of Kinetix (Majina halisi ya wanakundi ni Beston Shaban na Amani Hamisi), amabao wamepata zawadi ya pesa taslimu shilingi za kitanzania  1,000,000/= (Milioni moja)
Mshindi wa pili ni Nadzz Lilbeast (Nadeem Nizar), mshindi wa tatu ni Tafa Makuzi, Mshindi wa nne ni Editoo Kinywele (Idris Hamza) na Mshindi wa tano ni Angels’ (Angel Nyigu na Abdully Ally). Washindi wote wata wakilisha Mkoa wa Dar es Salaam Katika shindano la Kitaifa April 2017. Pamoja na fedha taslimu pia washindi walipata medali za dhahabu na silva kuanzia mshindi wa kwanza hadi wa tano
Baada ya Dar es Salaam, Dance Battle Zone litahamia katika mkoa wa Dodoma mwezi Septemba, ikifuatiwa na mkoa wa Arusha mwezi October na Zanzibar itakuwa ni mwezi December 2016
Lengo la shindano ni kupata mshindi atakayewakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia ya UDO World Street dance Championships, yatakayo fanyika huko Glasgow Scotland, mwakani mwezi kama huu wa August 2017.
UDO East Africa ina sajili washiriki 20 kila mkoa litakapo fanyika shindano la dance battle zone. washiriki watashindana kwa round nne kwa mwezi, yaani mara moja kwa wiki. Mshindi wa kwanza wa kila Mkoa atazawadiwa pesa taslimu Sh Milioni 1 ya kitanzania, pamoja na medali, mshindi wa pili hadi wa tano watapata medali na fursa ya kushiriki shindano la kitaifa. Ambapo mshindi wa kitaifa atapata fursa ya kushiriki shindano la dunia huko Glasgow Scotland, vigezo na masharti kuzingatiwa. Kila mshiriki wa dance battle zone atapewa cheti cha ushiriki.
Tunatoa wito kwa vijana wote wenye vipaji vya kucheza muziki wajitokeze na kushiriki shindano hili adhimu, fomu zinapatikana katika tovuti yetu ya www.udoeastafrica.com, pia katika ukumbi wa Maisha Basement, na Ofisi zetu zilizopo Kinondoni Road, mkabala na Bakwata. Dance ni kipaji, dance ni ajira, kuwa star kupitia dance battle zone.
Shindano hili linaletwa kwenu na UDO East Africa, kwa kushirikiana na Maisha Basement, Haak Neel Production, Mwakoba Associate, chini ya usimamizi wa Baraza la Sanaa la Taifa – BASATA.
UDO East Africa inawakaribisha wadau wote  wanaopenda kushiriki na kudhamini shindano la Dance Battle Zone almaarufu kama Mpambano wa Dance. Wasiliana nasi kupitia barua pepe; info@udoeastafrica.com , simu namba; +255 653 88 44 81

0 maoni:

Chapisha Maoni